Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Freddy Michael ameshindwa kujiunga na USM Alger ya Algeria kwa kigezo cha kutowahi kuchezea timu ya taifa, lakini mwenyewe amezima uvumi kwamba yupo nchini akivizia dirisha dogo ili ajiunge na Yanga kuchukua nafasi ya Kennedy Musonda.
Inadaiwa ili acheze soka la kulipwa Algeria ni lazima angalau angekuwa amepita timu za taifa japo ile ya vijana, na Freddy hajawahi kufanya hivyo na kukwamisha dili lake USM Alger.
Straika huyo amerudi Dar na kuungana na mastaa wa Yanga aliojifua nao na taarifa zikidai Yanga inamendea huduma yake, ili kumsajili dirisha dogo, ikielezwa huenda itaachana na Musonda aliyecheza dakika 1116 akifunga mabao matano, asisti mbili katika mechi 22.
Alipohojiwa na chombo na chombo kimoja cha habari hapa nchini, alisema Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kutaka huduma wakati akiwa Green Eagle, kabla ya Simba kupindua meza.
“Mimi ni mchezaji huru kwa sasa. Nipo tayari kuitumikia klabu yoyote itakayonihitaji, ila iwe na programu nzuri ya kunifanya nizidi kuwa bora.”
[…] wa zamani wa Simba, Freddy Michael ambaye alikuwapo uwanjani akiishuhudia timu yake ya zamani ikimkanda Mwarabu mabao 3-1 na kufuzu […]