Home Habari za Yanga Leo YANGA YASUKA KIKOSI…MBAYA WA SIMBA AREJESHWA KUNDINI

YANGA YASUKA KIKOSI…MBAYA WA SIMBA AREJESHWA KUNDINI

HABARI ZA YANGA-Injinia Hersi

KIKOSI cha Yanga kwa kundi la pili limepaa leo kuifuata CBE SA ya Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kabla ya kung’oa Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said akaunda jeshi jipya la kikosi kazi chenye sura za rekodi.

Injinia Hersi ameunda kamati mpya ya mashindano yenye watu nane akiendelea kumuamini Rodgers Gumbo aliyerejeshwa kama Mwenyekiti wa Kamati hiyo akiwa na rekodi ya maana.

Yanga ile iliyosumbua ikichukua mataji na kufanya vizuri Afrika, kamati hiyo ilikuwa inaongozwa na Gumbo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

Nyuma ya Gumbo amerejeshwa pia Lucas Mashauri atakayeendelea kuwa makamu ambaye alikuwa na na mwenyekiti wake ikichukua mataji hayo ya ndani tisa kwa misimu mitatu.

Ndani ya kamati hiyo wamo wajumbe sita wakiwemo watu wazito wawili Seif Ahmed ‘Seif Magari’ na swahiba wake, Davis Mosha ambao ni vigogo wa muda mrefu ndani ya timu hiyo.

Mbali na wawili hao wengine ni Pelegrinius Rutayuga,injinia Mustapha Himba, Majid Suleiman wakati sura mpya ikiwa moja ya Omary Kimosa.

Seif Magari amewahi kuongoza kamati kamati hiyo wakati wa utawala wa Marehemu Yusuf Manji kwa mafanikio makubwa, huku Mosha akiwahi kuwa makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga chini ya uongozi wa marehemu Imani Madega.

Taarifa za ndani ambazo Mwanaspoti imezinasa kwa uhakika ni kwamba kamati hiyo tayari ilishaanza kazi kimyakimya ikiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha timu hiyo inakwenda kutetea mataji yao ya ndani lakini pia kuhakikisha Yanga inafika mbali katika Ligi ya Mabingwa.

Nusu ya vigogo hao watashuka nchini Ethiopia kuhakikisha wanaendelea ubabe wao baada ya kuwang’oa Vital’O ya Burundi.

SOMA NA HII  TIMU YA WIKI CAF...SIMBA SC WAWILI...KAPOMBE NA CHAMA NDANI