HABARI ZA YANGA
Habari za Yanga Leo

YANGA YATUA ADDIS ABABA MUDA HUU

Abubakar September 12, 2024 11:52 am

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga SC wamewasili salama mjini Addis Ababa tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili dhidi ya CBE.

Yanga SC itashuka uwanjani keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa kuvaana na CBE FC kabla ya kurudiana nao wiki ijayo na mshindi wa jumla kutinga makundi.

Yanga ikitaka kuandika rekodi ya kufika hatua hiyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya msimu uliopiota kutinga baada ya miaka 25 kupita na kwenda hadi robo fainali kabla ya kutolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

MECHI YA YANGA NA CBE KUPIGWA ABEBE BIKILA SIMBA HAJAKATA TAMAA KWA MPANZU…DILI LAO LIMEFIKIA HUKU