Home Habari za Yanga Leo YANGA YATUA KWA MAKUNDI ETHIOPIA…WAHABESHI WAINGIA UBARIDI

YANGA YATUA KWA MAKUNDI ETHIOPIA…WAHABESHI WAINGIA UBARIDI

HABARI ZA YANGA

Yanga itatua nchini Ethiopia kwa makundi tofauti ambapo hapa unavyosoma Mwanaspoti kundi la wachezaji waliokuwa nchini Ivory Coast na kikosi cha Taifa Stars limeshatua nchini humo na kupokelewa kisha baadaye kundi la pili ni lile litakalotoka hapa nchini kisha watafuasta kipa Djigui Diarra na kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz KI na mshambuliaji Prince Dube.

Tayari Yanga ilishawatanguliza watu wawili akiwemo Mkurugenzi wa Mashindano, Ibrahim Mohammed Ethiopia kuandaa taratibu zote za awali.

Yanga itashuka uwanjani keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa kuvaana na CBE kabla ya kurudiana nao wiki ijayo na mshindi wa jumla kutinga makundi.

Yanga ikitaka kuandika rekodi ya kufika hatua hiyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya msimu uliopiota kutinga baada ya miaka 25 kupita na kwenda hadi robo fainali kabla ya kutolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

SOMA NA HII  GAMONDI AIPASUA CAF...KUELEKEA MCHEZO WA PILI ETHIOPIA