Home Habari za Simba Leo KWA UNDANI HAWA HAPA WAPINZANI WA SIMBA CAFCC.

KWA UNDANI HAWA HAPA WAPINZANI WA SIMBA CAFCC.

HABARI ZA SIMBA-AL AHL TRIPOLI

AL AHLI TRIPOLI Kwa Lugha ya Malkia Elizabeth wanafahamika kama National Sport Club kutoka jiji la Tripoli katika nchi ya Libya kwa Gadaffi, kwa wasifu ni klabu ya pili kwa mafanikio kwenye nchi ya Libya kwa ujumla nyuma ya Al-Ittihad.

Uwanja wa Tripoli Stadium ndio uwanja wao wa nyumbani klabu ya Karne ndio jina lao la utani  (Club of century) miaka 73 tangu ianzishwe mwaka 1750 September 19, Kijani jezi yao ya nyumbani na Away wanatumia White colour.

Msimu 2023/24 nafasi ya tatu kwenye ligi kuu ya Libya ndio imewapa kibali cha kushiriki michuano ya CAF confederation msimu huu hatua ya awali waliwaondosha Uhamiaji ya Zanzibar na kizingiti kingine ni Mnyama mkali wa mwituni Simba Sport Club kwenye kuwania kucheza group stage CAF confederation Cup this season.

Kwenye michuano hii ya CAF confederation Cup mwaka 2022 ndio mwaka ambao Al Ahli Tripoli walifanya vizuri zaidi baada ya kucheza Semi Final ya mashindano hayo lakini kwa ujumla hawana rekodi nzuri kwenye michuano hii ukiachana na ile Robo final ya mwaka 2017 kwenye CAF Champions league.

Kwa profile ya Simba kwenye michuano ya Africa hasa kwenye CAF Champions league Al Ahli Tripoli sio mpinzani mgumu kwao kwani walishacheza hatua kama hizi mara nyingi sana japo level ya michuano ni tofauti lakini bado sio mechi ngeni kwa Simba kwasababu ya experience yao kwenye hizi stage.

Kwenye Football chochote kinawezekana japo ugumu upo hivyo timu bora ambayo itazicheza mechi mbili kwa ubora mkubwa basi itacheza hatua ya makundi CAF confederation Cup.

SOMA NA HII  KIPIGO KUTOKA KWA WAARABU CHAMCHEFUA KOCHA MAKI....AWAPA MAKAVU LIVE MASTAA WAPYA...CHAMA AHUSISHWA...