Home Habari za Simba Leo MTU WA KUCHUNGWA ZAIDI AL AHLI VS SIMBA.

MTU WA KUCHUNGWA ZAIDI AL AHLI VS SIMBA.

habari za simba-Mabululu

MNYAMA Simba inatakiwa kuwa makini sana na mshambuliaji wa Tripoli, Agostinho Cristóvão Paciência, maarufu kama Mabululu ambaye amekuwa akiitumikia timu ya Taifa ya Angola kutokana na kiwango cha juu na uzoefu ambao amekuwa nao kwenye michuano ya kimataifa Afrika.

Mabululu ambaye ameshazichezea timu kadhaa kubwa Afrika kama Al Ittihad ya Misri, Petro de Luanda na Libolo, ameshacheza timu ya Taifa ya Angola michezo 36 na kufunga mabao 12 akiwa kati ya wachezaji waliocheza michezo michache na kufunga mabao mengi kwenye timu hiyo.

Kocha wa Simba Fadlu Davids, alisema wamejiandaa vizuri kuwakabili Al Ahli Tripoli wakiwa wamekamilisha sehemu kubwa ya maandalizi yao.

“Al Ahli Tripoli ni timu nzuri na imekuwa na historia ya kufanya vizuri kwenye mashindano haya huko nyuma. Hata hivyo, sisi ni timu kubwa naamini tunaweza kufanya mambo makubwa kwenye mchezo huu wa Jumapili ijayo.”

SOMA NA HII  SIMBA YASAJILI MCHEZAJI WA AZAM FC...ANAJUA BALAA