Home Uncategorized ABDI BANDA YUPO SALAMA HANA CORONA

ABDI BANDA YUPO SALAMA HANA CORONA

IMEELEZWA kuwa beki wa Highlands Park ya Afrika Kusini, Abdi Banda ameruhusiwa kurejea mazoezini baada ya kungundulika kwamba hana ugonjwa wa Corona.

Banda alisimamishwa kuendelea kujiunga kwenye mazoezi na wachezaji wenzake baada ya kuhisiwa kwamba hueda ameathirika na Corona.

Baada ya kufanyiwa vipimo vimeonyeshwa kwamba hana maambukizi ya Corona hivyo nyota huyo Mtanzania yupo salama.


Rafiki yake wa karibu kutoka Johannesburg amethibitisha na kusema:- “Ni kweli lakini isingekuwa rahisi kuzungumza kabla ya kupata uhakika wa majibu lakini tunashukuru yuko salama.


 “Unajua alikuwa anakohoa sana, hadi timu yake wakasema apumzike maana pia alikuwa na mafua. Lakini majibu yametoka na kila kitu safi na ameruhusiwa kuanza mazoezi.

“Akitulia atazungumza lakini kiana alikuwa na hofu pia, ndio maana alitaka kwanza kupata uhakika wa majibu.”

 

SOMA NA HII  SVEN VANDENBROEC ATAJA SABABU YA KUMUACHA BONGO MORRISON