Home Habari za Yanga Leo AZIZ KI, MZIZE WANAHITAJIKA ZAIDI WYDAD…ENG HERSI AFUNGUKA

AZIZ KI, MZIZE WANAHITAJIKA ZAIDI WYDAD…ENG HERSI AFUNGUKA

Habari za Yanga-Aziz Ki na Mzize

Klabu ya Wydad Casablanca imeongeza ofa kubwa zaidi ya $200K zaidi ya Tsh milioni 541, kwenda Yanga ili kumpata Clement Mzize kwa msimu 2025/26 baada ya ofa ya awali ya dola 100,000 (Tsh milioni 270,000) pamoja na dau jingine kwa ajili ya Aziz KI.

Ofa yao ina kipengele cha Yanga kulipwa jumla ya $500k (Tsh bilioni 1.3) kutokana na Performance yake itakavyokuwa. Yanga wamepanga kuikataa ofa hiyo. Wanataka $1m (Tsh bilioni 2.7).

Akizungumzia hilo, Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said amesema; β€œKila mchezaji anayecheza Yanga anatakiwa na timu nyingine Afrika. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu tuna wachezaji bora sana katika kikosi chetu.

β€œMokwena kocha amenipigia simu personally wakati tunacheza na TX Galaxy nchini Afrika Kusini, niko jukwaani akizungumzia kuhusu wachezaji wetu. Amemtaja Mzize ingawa pia anamtaka Aziz kwa kiwango kikubwa. Sisi tunaangalia kilicho bora ambacho kitakuja kwa maslahi ya mchezaji na klabu,” amesema Hersi.

β€œWalid Mzize ni tegemeo la taifa letu. Makocha wote wawili wa Yanga [Nabi na Gamondi] wamempa nafasi. Kwa sasa yuko kwenye mikono salama zaidi akiwa na jezi ya Yanga na ana mengi ya kujifunza na hapa ndio mahala sahihi kwake kwa maslani ya timu yetu ya Taifa pia,” Eng Hersi Said

SOMA NA HII  WAFAHAMU MARUNO GALLANTS WAPINZANI WA YANGA CAF....WANAHALI NGUMU KILA KONA....