Home Habari za Yanga Leo YANGA WALIVALIA NJUGA SAKATA LA YUSUPH KAGOMA…FOUNTAIN GATES WAWAKATAA KWEUPE

YANGA WALIVALIA NJUGA SAKATA LA YUSUPH KAGOMA…FOUNTAIN GATES WAWAKATAA KWEUPE

HABARI ZA SIMBA-KAGOMA

MKURUGENZI wa Sheria wa Yanga, Simon Patrick amethibitisha kuwa timu yao ilikamilisha mchakato wa kumsajili Yusuph Kagoma mwezi Machi 2024 kutoka klabu ya Fountain Gate.

Akizungumza wanahabari mapema leo, Simon amesema mazungumzo kati ya Yanga na Fountain Gate kwa ajili ya usajili wa Kagoma yalianza Machi 3, 2024

“Yanga ilipewa masharti na Fountain Gate ya kulipa Milioni 30 kumnunua Kagoma. Baada ya makubaliano ya klabu, pande mbili ziliingia mkataba ya mauziano ya mchezaji”
Yusuph Kagoma

“Mkataba halali ulisainiwa na pande mbili. Yanga ilipaswa kulipa fedha kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ikamilishwe kabla ya April 30 na Awamu ya pili ikamilishwe kabla ya Juni 30

Yanga ililipa fedha zote Milioni 30 kabla ya April 30 na Machi 27, 2024 Yanga ilimtumia Kagoma tiketi ya ndege kutoka Kigoma kuja Dar es salaam kwa ajili ya mazungumzo.

 

Habari za yanga-

Mpaka sasa tunaongea Yusuph Kagoma ni mchezaji halali wa Yanga Sc tulimsaini miaka mitatu na tukamtumia hadi tiketi ya ndege kutoka Kigoma nakuja Dar es salaam kuungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu huu 2024 – 2025” amesema Patrick Saimon, Mwanasheria wa Yanga

Kwa upande wa Fountain Gates FC ambao ndio walimuuza Kagoma kwenda Simba, wamesema kwamba Yanga walivunja makubaliano ya mkataba wao wa kwanza.

“Yanga hawakulipa kwa wakati, Million 30 ilipaswa kulipwa awamu mbili na hawakufanya hivyo”- Wakili wa Fountain Gate.

SOMA NA HII  MFAHANU REFA MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI AFRIKA...ANAYECHEZA MASHINDANO MAKUBWA