Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba, Ahmed Ally amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa timu yao iko salama licha ya ‘purukushani’ zilizojitokeza uwanjani baada ya mchezo dhidi ya Al Ahly Tripoli uliopigwa jana huko Libya
Baada ya mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, mashabiki wa Al Ahly Tripoli walifanya vurugu uwanjani kwa kuwarushia chupa wachezaji wa Simba pamoja na waamuzi
Ahmed amesema timu ililazimika kukaa uwanjani kwa takribani dakika 40 kabla ya kupanda basi kuelekea hotelini
“Tunashukuru tuko salama pamoja na vurugu zilizojitokeza, tumerejea hotelini salama kabisa”
“Hivyo tulikaa uwanjani kama dakika 40 ndipo tukapanda basi kuelekea hotelini. Kulikuwa na tukio la golikipa wetu Aishi Manula kushambuliwa wakati tunatoka jukwaani kuelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo, lakini tunashukuru nae hakupata madhara yoyote”
“Manula alishambuliwa na moja ya maafisa wa usalama katika tukio la kushangaza kwani ni wao waliotushauri tuende katika vyumba vya kubadilishia nguo tusubiri vurugu zutulie,” alisema Ahmed
Simba inatarajiwa kuondoka leo kurejea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ambao utapigwwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumapili ijayo.
[…] ya pili katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, kocha mkuu wa JKT Tanzania, Ahmed Ally amezipa mbinu timu […]