HABARI ZA YANGA-MTASINGWA
Habari za Yanga Leo

HATIMAYE MTASINGWA AJIBU KUHUSISHWAA NA YANGA

Abubakar September 19, 2024 11:51 am

KIUNGO wa Azam FC Adolf Mtasingwa, amejibu ule uvumi wa taarifa za yeye kujiunga na Yanga katika dirisha kubwa la usajili.

“MUDA ndio muamuzi wa kila jambo. Mengi yalizungumzwa juu yangu wakati wa dirisha la usajili, lakini wakati umeamua mimi kuwa hapa nilipo,”

Mtasingwa ambaye ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia Azam FC amethibitisha kuwa ni kweli alikuwa na ofa kutoka Yanga lakini amefanya uamuzi sahihi kubaki Chamazi kutokana na klabu hiyo kumuamini na kuhusu Jangwani, “labda wakati mwingine”. Adolf Mtasingwa.

Katika dirisha kubwa usajili kulisambaa taarifa za kiungo huyo  kuhitajika na Yanga,  ambapo ilielezwa kuwa mchezaji huyo alishasaini mkataba wa awali na Yanga na atajiunga nao dirisha dogo la usajili.

AL AHLI WAINGIA UOGA…WAKODI ULINZI MZITO YACOUBA SOGNE…BADO ANAUJUA SANA MPIRA