Habari za Simba Leo

SIMBA YAAMBULIA MEDALI…YANGA YASHINDWA KUTWAA NDOO

Abubakar October 5, 2024 9:00 pm

Timu ya wanawake ya Simba SC, Simba Queens imefanikiwa kushinda nafasi ya tatu baada kuichakaza bila huruma magoli manne bila majibu timu ya CEASIAA katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii kwa timu za mpira wa miguu za wanawake.

Simba Queens ilitolewa na Yanga Princes hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penati huku CEASIAA akitolewa na JKT Queens.

Baada ya mchezo huo, fainali inawakutanisha Yanga Princes na JKT Queens katika uwanja wa KMC hii leo.

YANGA YAPORWA KOMBE UWANJANI…JKT QUEENS WABABE FEISAL AIKATAA MIL 50  YA AZAM FC….WAMUWEKEA MAMILIONI MEZANI