Home Meridianbet LIGI KUBWA BARANI ULAYA KUKUPA MKWANJA KUPITIA MERIDIANBET…

LIGI KUBWA BARANI ULAYA KUKUPA MKWANJA KUPITIA MERIDIANBET…

Meridianbet

Klabu ya Fc Bayern Munich mabingwa wa muda wote nchini Ujerumani wanakabana koo na klabu ya Rb Leipzig kunako ligi kuu ya soka nchini Ujerumani Bundesliga kutokana na namna msimamo wa ligi hiyo ulivyo mpaka sasa.

Mpaka sasa kwenye msimamo wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga Bayern Munich wanaongoza msimamo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, Lakini wamelingana alama na klabu ya Rb Leipzig wote wakiwa na alama 14 baada ya kucheza michezo sita kila mmoja.

Klabu ya Bayern Munich chini ya kocha mpya Vicent Kompany imefanikiwa kuanza msimu vizuri tofauti na msimu uliomalizika, Ambapo hawakua na msimu mzuri wakimaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu ikiwa ni baada ya miaka mingi sana walikua hawajamaliza ligi kwenye nafasi hiyo.

Bayern Munich kwenye michezo sita mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja ambapo wameshinda michezo minne, Huku wakisuluhu michezo miwili ambapo ni sawa na klabu ya Rb Leipzig ambao na wao hawajapoteza mchezo mpaka sasa kwenye ligi hiyo wakionekana kwenda jino kwa jino na Bayern.

Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko mahala pengine, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.

Wakati msimu ukianza vizuri kwa vilabu vya Bayern Munich na Rb Leipzig mambo yamekua tofauti kwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo klabu ya Bayer Leverkusen, Ambapo wanaonekana kuuanza msimu kwa kusuasua ikiwa mpaka sasa wakiwa nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wakikusanya jumla ya alama 11 kwenye michezo mitano wakishinda michezo mitatu, Kusuluhu miwili na kufungwa mchezo mmoja ikiwa sio takwimu nzuri ukilinganisha na namna ambavyo walianza msimu uliopita.

SOMA NA HII  ODDS ZA KUTOKA NA MKWANJA WA MERIDIANBET KWA MECHI ZA LEO USIKU NI HIZI HAPA...