Habari za Simba leo
Habari za michezo

FT:- SIMBA 4-0 KMC….AHOUA ALIVYOWAUA YANGA KILELENI….

admin November 6, 2024 9:43 pm

Timu ya Simba Sports Club imefanikiwa kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Alianza kiungo Awesu Ally Awesu kuiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 25, kabla ya kiungo mwingine, Muivory Coast, Jean Charles Ahoua kufunga mara mbili dakika ya 38 kwa penalty na 69 na kiungo mwingine, huku bao lingine likifungwa winga Edwin Balua dakika ya 66.

Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 25 katika mchezo wa 10 na kupanda kileleni, ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mechi moja mkononi.

Katika mchezo huo Jean Charles Ahoua amechaguliwa nyota bora wa mchezo baada ya kuhusika kwenye mabao mawili pamoja na kuonyesha kiwango safi.

TAJIRIKA NA UEFA LEO NDANI YA MERIDIANBET…ODDS ZA UHAKIKA HIZI HAPA.. CAMARA vs MASTAA SIMBA USO KWA USO TANZANIA IKIUMANA NA GUINEA…SHOW IKO HIVI…