Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WASUDANI LEO….KOCHA MPYA YANGA KUINGIA NA STAILI HII YA...

KUELEKEA MECHI NA WASUDANI LEO….KOCHA MPYA YANGA KUINGIA NA STAILI HII YA KIJERUMANI..

Habari za Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Yanga, Sead Removic amesema tayari ameshawasoma Al Hilal Omdurman ya Sudan, sasa kazi alioanza nayo kubwa ni kuweka mipango sawa safu ya ulinzi na ushambuliaji kuwa makini katika mchezo huo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kumaliza shughuli.

Removic amesema kuwa itakuwa mechi yake ya kwanza tangu amekabidhiwa timu hiyo ikicheza dhidi ya Al Hilal ya Sudan utakaochezwwa leo Jumanne Novemba 26,uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam, hivyo ni lazima awe makini.

Amesema kazi kubwa aliyonayo ni kuwanoa mabeki wa Yanga wanaoongozwa na Bakari Mwamnyeto, Yao Koussi, Dickson Job, Ibrahim Bacca kuhakikisha wanafanikiwa kuwazuia washambuliaji wa Al Hilal, huku safu ya viungo washambuliaji, ya kina Clatous Chama, Stephane Aziz Ki, na mastraika, Clement Mzize na Prince Dube, kila idara ifanye inayokusudiwa kwa ajili ya kusaka ushindi wa kwanza.

Hata hivyo amesema kwa kipindi kufupi ambacho amekabidhiwa timu hawezi kutengeneza kitu kikubwa, zaidi tu ya kuyaangalia makosa na ubora wa wapinzani wao na kuyafanyia kazi.

“Nimewaangalia Al Hilal namna wanavyocheza na nini watafanya , timu ngumu ipo timamu kimwili ila tayari nina mpango namna ya kucheza na tunafanyia mazoezi, Inshallah kila kitu kitakuwa sawa, “ amesema.

Removic amesema kikosi kipo imara na ana imani ya wachezaji kufanyia kile anachotoa kwenye mazoezi na kupata matokeo mazuri katika mchezo wa nyumbani.

Naye Dickson Job amesema kuna mabadiliko ya benchi la ufundi lakini mbinu na mipango ni ile ile ya kushinda mechi ya Jumanne Novemba 26, dhidi ya Al Hilal.

“Haitakuwa mechi rahisi ukizingatia wapinzani wetu wako vizuri na kocha amewaangalia na kuona ubora wake na kutueleza tunahitaji kuingia vipi,” amesema.

SOMA NA HII  BAADA YA KUICHAPA SIMBA, SENZO AWAPIGA MKWARA WACHEZAJI YANGA