Home Habari za michezo MASHINE HII YA SIMBA KUSEPA DIRISHA DOGO….

MASHINE HII YA SIMBA KUSEPA DIRISHA DOGO….

Habari za Simba leo

MABOSI wa KMC wapo katika mazungumzo ya kupata saini ya nyota wa Simba, Salehe Karabaka kwa mkopo wa miezi sita baada ya kutokuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo chini ya kocha mkuu raia wa Afrika Kusini, Fadlu Davids.

Taarifa kutoka Simba zinasema kuwaKarabaka ni miongoni wa wachezaji watakaotolewa kwa mkopo dirisha hili dogo la usajili litakalofunguliwa Desemba 15, ili akapate nafasi zaidi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

“Ni kweli KMC wameonyesha nia ya kumhitaji lakini sio wao pekee kwa sababu zipo klabu nyingine zinazomhitaji pia, tunachotaka au kukizingatia ni kumpeleka timu itakayompa nafasi ya kucheza zaidi kikosini,” kilisema chanzo chetu.

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa KMC, Daniel Mwakasungula alisema hawezi kuzungumzia suala la mchezaji huyo, ingawa kama viongozi walishaanza taratibu zote za kukamilisha baadhi ya wachezaji, kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi.

“Nikuibie siri tu sisi tayari tumeshamaliza kusajili na kilichobaki ni kuwatangaza tu siku dirisha litakapofunguliwa, siwezi kusema ni nani na nani ila mashabiki zetu watarajie usajili uliokuwa bora na makini sana,” alisema Mwakasungula.

Karabaka aliyejiunga na Simba katika dirisha dogo la Januari mwaka huu akitokea JKU SC ya Zanzibar, ameshindwa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani uliopo, jambo linalomfanya afunguliwe milango ya kutokea.

Nyota huyo aliyesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu, tangu ajiunge na timu hiyo amefunga bao moja tu la Ligi Kuu Bara alilolifunga katika ushindi wa kikosi hicho wa mabao 2-0, dhidi ya Mtibwa Sugar, Mechi ikipigwa Mei 3, 2024.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MAKABI KUWA MBADALA WA MAYELE YANGA...MAKOCHA WAVUNJA UKIMYA...