Home Habari za michezo ZA NDAANI KABISA…..YANGA WAMTUPIA ZIMBWE Jr OFA YA KIBABE…..MWINGINE ANAYETAJWA HUYU HAPA..

ZA NDAANI KABISA…..YANGA WAMTUPIA ZIMBWE Jr OFA YA KIBABE…..MWINGINE ANAYETAJWA HUYU HAPA..

Tetesi za Usajili Leo

YANGA imeendelea na mipango ya kukisuka kikosi kwa ajili ya mechi za michuano mbalimbali inatoshiriki, ikielezwa imerudi kwa kipa wa Pamba Jiji, Yona Amos ili kumnasa kupitia dirisha dogo, huku jina la Abuutwalib Mshery akitajwa ndilo litakalokatwa ili kumpisha kipa huyo anayeidakia pia Taifa Stars.

Awali Yanga ilikuwa ikimnyemelea kipa huyo aliyekuwa Tanzania Prisons, kabla ya kumkosa na kuangukia kwa kipa wa Ihefu, Abubakar Khomeiny, lakini kutokana na kipa huyo kushindwa kumpa changamoto za kutosha Diarra Djigui ndiyo maana mabosi wamemrudi tena Amos.

Taarifa  kutoka kwa mtu wa karibu wa Amosi, zinasema kwa sasa mazungumzo yanayoendelea baina ya kipa huyo na uongozi wa Yanga na kama mambo yataenda kama inavyopangwa basi muda wowote dili lake linaweza kutiki.

“Viongozi wa Yanga wamerudi tena kuhitaji huduma ya Amos, kuna mazungumzo yanaendelea kuona kama itawezekana kumsajili dirisha dogo, ninachokiamini lolote linaweza likatokea,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kuna mambo hayakwenda sawa ndiyo maana dili lake mwanzoni mwa msimu likafeli, awamu hii naona kuna uwezekano mkubwa kwa sababu, Pamba inahitaji baadhi ya wachezaji kwa mkopo kutoka Yanga, hivyo haiwezi kuweka ugumu kumwachia kipa huyo.”

Yanga hivi karibuni imemtangaza beki Israel Mwenda kutoka Singida Black Stars atakuwa sehemu ya kikosi hicho, pia inafukuzia saini ya kiungo Micky Harvey anayecheza FC Lupopo ya DR Kongo, ukiachana na huyo inaelezwa imempa ofa nono beki Mohamed Hussein ‘Zimbwe’ wa Simba, kuliko ile iliyowekwa na klabu yake.

Taarifa za Zimbwe sio ngeni kutajwa Yanga, kwani msimu uliopita kuna taarifa zilikuwa zinamhusisha yeye na beki Shomari Kapombe kuhitajika na klabu hiyo.

SOMA NA HII  MKUTANO MKUU YANGA : MANJI ATUA NA KUPAGAWISHA WANACHAMA