Home Meridianbet KITUO CHA WATOTO YATIMA UMRA CHAFIKIWA NA BITTECH….

KITUO CHA WATOTO YATIMA UMRA CHAFIKIWA NA BITTECH….

Meridianbet

Kama ilivyo ada katika kuendeleza uhusiano na jamii kampuni ya Bittech leo hii wakishirikiana na KMC FC yagawa Madaftari, Penseli, na Mabegi kwa Watoto Yatima wa Umra

Leo hii Kampuni ya Bittech wamefanya tukio la kijamii kwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto yatima wa Umra kinachopatikana Magomeni kama sehemu ya juhudi za kuunga mkono maendeleo ya elimu na ustawi wa watoto katika jamii.

Zoezi hili lilifanyika katika kituo cha watoto yatima cha Umra, ambapo watoto walipokea madaftari, penseli, mabegi ya shule, na vifaa vingine muhimu kwa ajili ya masomo yao.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhariri wa Bittech, Bi Nancy Ingram alisema, “Kama kampuni, tuna furaha kubwa kuona watoto hawa wakiwa na vifaa vya shule vitakavyowawezesha kufuata masomo yao kwa urahisi. Hii ni sehemu ya dhamira yetu ya kusaidia watoto yatima na kuwekeza katika elimu, ambayo ni ufunguo wa mafanikio ya kesho.”

Watoto hao walionekana furaha na shukrani kwa msaada huo, huku wakielezea matumaini yao kuwa vifaa walivyopokea vitawasaidia kuwa na mafanikio katika masomo yao. Viongozi wa kituo cha watoto yatima cha Umra walielezea shukrani zao kwa kampuni ya Bittech na KMC FC kwa msaada mkubwa walioutoa, wakisema kwamba msaada huu utaleta mabadiliko katika maisha ya watoto hao.

Ukiachana na hilo kumbuka pia kubashiri na Meridianbet ambapo odds kubwa na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.

Kampuni ya Bittech na KMC FC wameahidi kuendeleza juhudi hizi za kijamii, na wataendelea kushirikiana katika miradi inayolenga kuboresha maisha ya watoto yatima na jamii kwa ujumla. Hii ni hatua nyingine muhimu katika kuleta mabadiliko chanya na kusaidia maendeleo ya elimu nchini.

SOMA NA HII  MERIDIANBET YATOA JEZI KWA JOGOO VETERAN....