Home Habari za michezo BAADA YA KUWA ‘MCHOMAJI’ KWA MECHI ZA HIVI KARIBUNI….CHE MALONE AANGUA KILIO...

BAADA YA KUWA ‘MCHOMAJI’ KWA MECHI ZA HIVI KARIBUNI….CHE MALONE AANGUA KILIO SIMBA…

Habari za Simba leo

BEKI wa kati wa Simba, Che Malone leo amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kutokana kosa alilolifanya jana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos ya Angola.

Malone ameomba msamaha huo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiahidi kurekebisha makosa yake na kurudi akiwa imara.

Beki huyo raia wa Cameroon amekuwa mchezaji muhimu kikosini tangu msimu uliopita katika eneo la ulinzi akitumika kwenye mashindano yote ikiwamo yale ya Ligi Kuu na kimataifa.

Kwenye mchezo jana ambao Simba ilitoka sare ya 1-1 na kutinga roibo fainali, Malone alifanya kosa kurudisha pasi kwa kipa wake, Moussa Camara iliyowapa faida ya bao wapinzani wao.

“Ningependa kuomba samahani kwa familia nzima ya Simba kwa makosa niliyofanya ambayo yaliigharimu timu kwenye siku mbili muhimu za mechi. Nachukua jukumu kamili kwa matendo yangu na ninaelewa athari zake,” amesema Malone na kuongeza:

“Kuanzia sasa nimejikita kufanya kazi kwa bidii zaidi na kuboresha kiwango changu ili niweze kuchangia vyema mafanikio ya timu. Asanteni sana kwa msaada wenu wa dhati na kunitia moyo hata katika nyakati ngumu. Imani yenu kwangu inanipa nguvu ya kukua na kurejea nikiwa bora zaidi.”

Huu ni msimu wa pili kwa mchezaji huyo kucheza Simba akisajiliwa 2023 na tangu hapo aliingia kwenye kikosi hicho na kushiriki michuano mbalimbali.

SOMA NA HII  BREAKING: RASMI LUIS MIQUISSONE ATAMBULISHWA AL AHLY YA MISRI