Home Habari za michezo TAKWIMU ZINAONGEA….HAPA NDIPO SIMBA WALIPOIPIGA BAO YANGA MSIMU HUU…

TAKWIMU ZINAONGEA….HAPA NDIPO SIMBA WALIPOIPIGA BAO YANGA MSIMU HUU…

Habari za Simba na Yanga

WAKATI jumla ya mabao 264 yakifungwa hadi kumalizika kwa mechi za mzunguko wa kwanza, Simba inaonekana ni hatari zaidi kufunga mabao wachezaji wake wanapokuwa ndani ya eneo la hatari, huku Yanga wakiwa nje ya boksi.

Kwa mujibu wa Takwimu , Simba inaongoza kwa kufunga mabao mengi ndani boksi, huku Yanga ikiongoza kwa mabao ya mbali.

Simba imepachika mabao 28 ndani ya eneo la hatari kati ya 31 ambayo imefunga mpaka sasa kwenye Ligi Kuu. Ni mabao matatu tu ambayo timu hiyo imefunga ikiwa nje ya boksi.

Watani zao wa jadi, Yanga wanafuatia kwa kufunga mabao ndani ya kisanduku cha hatari, wakipachika 26, huku Azam ikishika nafasi ya tatu, ikiwa na mabao 22 iliyoyafunga karibu na lango.

Nafasi ya nne imechukuliwa na Singida Black Stars, ikifunga mabao 20, Fountain Gate ya tano na mabao 18, Tabora United ikishika nafasi ya sita, ikiwa na 16 ndani ya boksi, Coastal Union ya saba na mabao yake 14, huku nafasi ya nane ikichukuliwa na Dodoma Jiji, ambayo ina 13 iliyoyafunga ndani ya kisanduku cha hatari.

Kwenye mabao ya nje ya boksi, Yanga inaongoza pamoja na timu za Fountain Gate na Mashujaa FC, ambazo zote zimepachika mabao sita nje ya boksi kila moja.

Timu zinazofuatia ni Simba, Tabora United, Azam FC, JKT Tanzania na Kagera Sugar ambazo kila moja imefunga mabao matatu, wachezaji wake wakiwa nje ya eneo la hatari.

Takwimu zinaonesha kuwa mabao hayo 264, yamefungwa katika michezo 127 iliyochezwa mpaka sasa, ambapo mechi 94 zimetoa washindi na 33 zimeishia kwa sare.

Katika michezo 94 ambayo timu zimeshinda, mechi 58 timu zimepata ushindi zikicheza nyumbani na mechi 36 zimetoa washindi zikicheza ugenini.

SOMA NA HII  MABEKI WAWILI WENGINE TENA WAONGEZA MKATABA SIMBA, WAUNGANA NA KAPOMBE, TSHABALALA