Home Habari za michezo KAMWE:- MAUMIVU HAYA YATAKUWA MARA MBILI KWETU…

KAMWE:- MAUMIVU HAYA YATAKUWA MARA MBILI KWETU…

Habari za Yanga leo

OFISA Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema maumivu ya kuondolewa kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika yawe darasa na sehemu ya kupambana wasije kuumia zaidi siku za usoni.

Kamwe amesema maumivu wanayopata kwa kuondolewa kwenye makundi wanaweza kuhisi makubwa na mazito, wanatakiwa kutumia nafasi hii kujiuliza na kujipanga kwa ajili ya kutetea mataji ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho (FA).

“Tukipoteza makombe yetu tuliyopata msimu uliopita, maumivu haya yatakuwa makali mara mbili au zaidi. maumivu haya yawe darasa na sehemu ya kupambana kufanya vizuri, tusije kuumia zaidi, tumegundua furaha yetu inawaumiza wapinzani wetu, basi tushikamane,” amesema.

Kamwe amesema sasa nguvu na akili zao wanatakiwa kuelekeza katika michuano iliyopo mbele yao ya Ligi Kuu na michuano ya kombe la FA kuhakikisha wanafanikiwa kutetea mataji hayo.

“Tunahitaji kufanya vizuri katika michezo yetu ya ligi kukusanya alama tatu kila mechi na kurejea kwenye nafasi yetu ya kuongoza ligi na kufanya vizuri michuano ya FA,” amesema Kamwe.

Yanga ilishuka dimba la KMC Complex, kwenye mchezo wa michuano ya kombe la Shirikisho la FA dhidi ya Copco FC, uliochezwa, Jumamosi, Januari 25 na kushinda kwa goli 5-0.

SOMA NA HII  KISA KUFUZU KOMBE LA DUNIA ...TIMU ZA TAIFA ZAJAZWA MABILIONI YA PESA...WAZIRI MKUU AFUNGUKA A-Z...