Home Burudani KUHUSU POSA YA AZIZ KI KWA HAMISA….UKWELI HUU HAPA….MAMA MZAZI AFUNGUA A-Z….

KUHUSU POSA YA AZIZ KI KWA HAMISA….UKWELI HUU HAPA….MAMA MZAZI AFUNGUA A-Z….

Habari za Yanga leo

MAMA wa msanii wa Bongo Flava na mjasiriamali, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga amesema mwanaye huwa hamfichi jambo lolote ikiwamo mahusiano yake na amekuwa mshauri wake kwenye kila jambo, huku akikiri kuna posa zimemfikia.

Kumekuwa na stori kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nyota wa Yanga, Stephanie Aziz Ki kutaka kumuoa Hamisa na tayari ameshapeleka posa kwa mama yake na mama wa msanii huyo na kufunguka ukweli kuhusu uhusiano wao na kama ni kweli walipanga kufunga ndoa mwezi huu wa Februari.

Mama Hamisa amesema amesikia mengi mitandaoni kuhusu wawili hao na kuhusu suala la posa kuletwa sio Aziz Ki pekee aliyeleta na ana rundo la posa kutoka kwa wanaume wengi walioonyesha nia ya kumuoa binti yake.

Anafunguka, hakuna posa yoyote aliyopokea kutoka kwa kiungo huyo mshambuliaji wa Yanga kama baadhi ya watu walivyozusha mitandaoni na hana taarifa za mwanae kama anataka kuolewa naye.

“Kiukweli mimi hapana, sijui habari za ndoa wala sijapokea posa ya huyo mchezaji, mie nasikia tu kama unavyosikia wewe na kuona kwenye mitandao, nami ndiye mama mzazi na Hamisa, na mwanangu Hamisa huwa hanifichi kitu chochote, tumezoea kuzungumza kila wakati na kupeana ushauri wa mambo mbalimbali, ila kwa hili kama lipo ningelijua tu,” amesema Shufaa.

Mama huyo alisema ni kweli amekuwa akipokea barua za posa za bintie, lakini hizo zinawahusu watu wengine na sio mchezaji huyo wa Yanga na wote wanahitaji kumuoa, lakini uchaguzi upo kwa Hamisa mwenyewe.

“Kuna wanaume wengi wamewahi kujitokeza kuomba ndoa na Hamisa, nimekuwa napokea posa nyingi sana na nimekuwa makini sana katika suala la mahusiano yake, ila chaguo la Hamisa la mwanamume ambaye atampenda jinsi alivyo bila kubagua chochote ikiwemo watoto wake wawili basi mimi nampa baraka zote, sababu wapo wanaume ambao wanampenda mwanamke tu bila kujali watoto aliowakuta nao mwanamke.”

Wiki hii Hamisa amezungumzwa katika mitandao ya kijamii baada ya video yake na Aziz KI, wakiwa Dubai wakiponda raha.

Pia wawili hao walichapisha jumbe za kimahaba kupitia kurasa zao za Instagram, zikionyesha wazi hisia zao za dhati.
Hamisa aliandika kwenye Instagram, “He is exactly the poem that I want to write,” akionyesha namna anavyompenda Stephanie Aziz Ki.

Kwa muda mrefu, wawili hao walikuwa wakikanusha uvumi wa kuwa pamoja, huku wakiepuka kujibu maswali ya mashabiki na vyombo vya habari kuhusu ukaribu wao.

Hamisa ana watoto wawili, Fantasy aliyezaa na Majizo na Dylan aliyezaa na Diamond Platnumz.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA KIWANGO CHA NGUSHI JUZI..NABI KAINAMISHA KICHWA KISHA AKASEMA HAYA...