UONGOZI wa Yanga umesema moja ya kipengele cha Kocha Mkuu anayeenda kukinoa kikosi cha timu hiyo ni kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kombe la Shirikisho FA.
Yanga wamemtangaza Kocha Mkuu Hamdi Miloud kutoka Singida Black Stars kuchukuwa nafasi ya Sead Ramovic aliyeondoka baada ya kupata ofa nzuri ya kukinoa kikosi cha CR Belouizdad ya Algeria.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Abdihamid Moallin amesema kila kocha anayekuja klabuni jukumu lake ni moja kutetea taji la ubingwa, makocha waliopita walifanya kazi zao vizuri na anaimani anayekuja atapita katika njia ambayo wametengeneza waliopita kuleta mafanikio katika klabu.
“Ukiwa na wachezaji kama hawa kila kocha anayekuja anakutana na kikosi bora, ninaimani ya kuendeleza mafanikio anayoyakuta na moja ya jukumu lake ni Yanga kupata matokeo chanya na kufikia malengo,” amesema.
Moallin alikaim nafasi ya kocha mkuu nkatika katika mchezo dhidi ya Ken Gold, amesema kikosi cha Yanga kipo vizuri, wameonyesha mchezo mzuri dhidi ya Ken Gold na kufanikiwa kushinda idadi kuwa na mabao.
Amesema ushindi wa mabao 6-1 ni vizuri kwa sababu mwisho wa msimu yatasaidia kuangalia idadi ya mabao ya kufunga baada ya kufanana kwa alama.