Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA CHASAMBI KUJIFUNGA JUZI…FADLU ASHINDWA KUJIZUIA..MSIMAMO WAKE HUU..

KUHUSU ISHU YA CHASAMBI KUJIFUNGA JUZI…FADLU ASHINDWA KUJIZUIA..MSIMAMO WAKE HUU..

Habari za Simba leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amemkingia kifua nyota wake, Ladack Chasambi kwa kusema anatakiwa kusaidiwa na sio kulaumiwa, kwa kosa la kujifunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Fountain Gate FC.

Simba imelazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo huo wakiwa ugenini wakati Wekundu hao walianza kupata bao la uongozi dakika 57 na 75 Chasambi akajifunga baada ya kurudisha mpira kwa kipa wake, Moussa Camara, uwanja wa Tanzanite Kwara, Babati.

Fadlu amesema ulikuwa mchezo mzuri, wakiufundi na mbinu, lakini haikuwa siku yao na bao la kujifunga la Chasambi hatakiwi kulaumiwa bali kusaidiwa ili ajifunze zaidi kupitia makosa hayo.

“Chasambi ni kijana mdogo anatakiwa kulindwa kwa ajili ya kukilinda kipaji chake, bado anahitaji kusimamiwa na kupewa moyo kwa sababu ni hazina ya Taifa na hatakiwi kupotezwa,” amesema.

Fadlu amesema kazi kubwa wanaendelea kuzungumza na nyota huyo kuendelea kumjenga na kumtengeneza kisaikolojia kwa ajili ya michezo ijayo ikiwemo dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.

Kikosi cha Simba kinarejea jijini Dar es Salaam baada ya kuvuna alama nne kwenye michezo miwili ya ugenini iliibuka na ushindi wa bao 3 -0 na Tabora United, Uwanja wa Al Hassan Mwinyi na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Fountain Gate.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTOKA SARE NA MBEYA CITY...MAKOCHA WAPYA AZAM WAVUNJA UKIMYA...WATAJA MABADILIKO...