BEKI tegemeo wa klabu ya Simba, Mohammed Hussein maarufu kama Zimbwe JR, ametamka kwa kujiamini kuwa kikosi cha msimu huu ni bora zaidi kuwahi kuchezewa tangu ajiunge na wekundu hao wa Msimbazi.
Akizungumza kwa msisitizo, Zimbwe JR amesema kuwa takwimu hazidanganyi licha ya kucheza kwenye vikosi vingi vya Simba, timu ya sasa imefanya makubwa kwa kufuzu hadi hatua ya nusu fainali ya mashindano ya kimataifa, jambo ambalo halijawahi kutokea kwa miaka mingi.
“Kuna Simba bora niliyowahi kuchezea, lakini hii ya sasa ni ya kipekee. Tumefuzu nusu fainali baada ya miaka mingi ya kujaribu kuandika historia. Mwaka 1993 ilikuwa ni historia inayozungumzwa sana lakini sasa nasi tumeandika yetu,” amesema kwa furaha.
Zimbwe JR amefichua kuwa mafanikio hayo hayakutokea kwa bahati nasibu. Anaeleza kuwa kila kitu kilianza tangu mechi ya kwanza walipowasili nchini Misri, ambapo walifanya kikao kizito na kocha wao Fadlu Davids.
“Mazungumzo kati yetu na kocha yalikuwa na uzito. Kocha alieleza malengo kutoka robo fainali hadi nusu fainali. Sote tulijitolea kupigania hilo, na leo hii tumefanikisha,” alisema beki huyo.
SOMA NA HII KISA 'MVUA YA MAGOLI'....MBEYA CITY WAPAZA SAUTI KUHUSU TABIA ZA SIMBA KWA MAGOLIKIPA...