Home Habari za michezo AHOUA, MUTALE ‘WAWATOA MATE’ KAIZER CHIEFS…..NABI ATUA BONGO KUSETI MIPANGO….

AHOUA, MUTALE ‘WAWATOA MATE’ KAIZER CHIEFS…..NABI ATUA BONGO KUSETI MIPANGO….

Haabri za Simba leo

KOCHA wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Nasredine Nabi ameondoka nchini na kumtimkia Ulaya kwa mapumziko, lakini hapa Tanzania alimuacha skauti wao mmoja maalum kwa ajili ya kuwaangalia viungo wawili wa Simba.

Nabi alipokuwa nchini kwa mambo yake binafsi alishuhudia mchezo wa Simba dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa pale KMC Complex, wekundu hao wakishinda kwa bao 1-0.

Baada ya mchezo huo alivutiwa na kiungo Ahoua kisha akatia neno kidogo  kumbe hakuishia hapo tu, bali alimpa kazi maalum skauti mkuu wa Kaizer, Thembela Tera Maliwa.

Maliwa alibakishwa hapa nchini kisha akasafiri hadi Manyara wakati Simba ikienda kucheza tena dhidi ya Singida BS katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kumuangalia tena Ahoua ambaye alifunga bao kali kwa mpira wa frii-kiki wakati timu hiyo ikilala kwa mabao 3-1.

Mbali na Ahoua pia Maliwa alikuwa na kazi ya kumuangalia tena vizuri, winga Mzambia Joshua Mutale ambaye ni kipenzi cha mabosi wake ambapo wawili hao wote walianza katika michezo yote miwili iliyopita dhidi ya Singida, lengo likiwa ni kuwapigia hesabu kuwasajili kwa msimu ujao.

MSIKIE NABI

Akizungumzia alivyoiona Simba katika mechi hiyo ya kwanza, Nabi alisema Wekundu hao hawakucheza kwa nguvu sana akiona ni kama walikuwa na uchovu wa mwisho wa msimu.

Hata hivyo, Nabi akizungumzia viwango vya wachezaji alionyesha kuvutiwa na Ahoua akisema kiungo huyo anacheza kwa utulivu na akili yake inafanya kazi vizuri kufanya uamuzi haraka uwanjani.

“Ndio nimeiona Simba wana timu nzuri, lakini sikufurahia sana kiwango chao nadhani labda kwa kuwa Ligi inakaribia kumalizika wana uchovu, hawajachangamka,” alisema Nabi ambaye pia jukwaani alikuwa na msaidizi wake Mrundi Cedric Kaze huku akiongeza;

“Wachezaji wa Simba ni wazuri, lakini kwangu mimi nimevutiwa sana na yule jezi namba 10 (Ahoua) ni kiungo mzuri anafanya mambo kwa uhakika na akili yake inafanya uamuzi kwa haraka.”

Ahoua aliyesajiliwa na Simba msimu huu kutoka klabu ya Stella Club d’Adjame ya Ivory Coast, anaongoza orodha ya wafungaji akiwa na mabao 15 na asisti nane katika Ligi Kuu Bara, huku katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika akifunga mabao matatu na jingine la FA.

SOMA NA HII  MABOSI SIMBA WATUA NYUMBANI KWA KINA PACOME...MIPANGO YATEKELEZWA KIMYA KIMYA