Home Habari za michezo YANGA YAJIANDAA NA PAMBA JIJI FC, PEDRO AWEKA MIKAKATI YA USHINDI

YANGA YAJIANDAA NA PAMBA JIJI FC, PEDRO AWEKA MIKAKATI YA USHINDI

0

KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Pedro Goncalves, ameamua kuanza kupanga mikakati maalumu ili kuhakikisha kikosi chake kinapata alama tatu katika mchezo ujao wa ugenini wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Pamba Jiji FC.

Yanga wanatarajiwa kusafiri hadi Mwanza kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa katika dimba la CCM Kirumba, wakiwa na lengo la kupata alama tatu muhimu zitakazowaweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

Hali hiyo inakuja baada ya Yanga kushindwa kuonyesha muendelezo mzuri katika michezo ya ugenini hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, ambapo waliambulia pointi moja tu.

Pedro ameeleza kuwa maandalizi ya timu yake kwa mchezo ujao yalianza mara tu baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mechi dhidi ya Tanzania Prisons, akiwahimiza wachezaji wake kuzingatia nafasi kubwa wanazopaswa kuonyesha mbele ya Pamba Jiji FC.

“Ligi ni kama mbio ndefu (marathon), tunatakiwa kuwa makini na kufanya maandalizi. Tulichofanya katika mchezo uliopita hatutaweza kufanya katika mchezo ujao,” amesema Goncalves.

Kocha huyo amesema maandalizi ya kila mchezo yanatofautiana kulingana na mpango wa mechi, na wanajipanga kuhakikisha wanavuna alama tatu muhimu kila mara, kwani malengo yao makuu ni kutetea ubingwa wa ligi.

Goncalves  ameeleza furaha yake kuona baadhi ya wachezaji wake waliokuwa majeruhi wameanza kurejea uwanjani, jambo ambalo limeongeza nguvu na ari ya kupambana kwa kikosi chote.