Habari za michezo

SAKATA LA DAMARO, HERSI AWEKA MAMBO WAZI, AITENGA YANGA

Vardo April 11, 2026 2:21 pm

RAIS wa Yanga, Hersi Said, ameweka wazi sakata linalomhusu kiungo wao Mohammed Damaro, akisisitiza kuwa klabu hiyo haihusiki kwa namna yoyote na suala la uraia wa mchezaji huyo.

Kauli hiyo imekuja kufuatia mjadala unaoendelea nchinj, ambapo baadhi ya mashabiki wamekuwa wakihoji uhalali wa uraia wa Damaro na namna alivyopata hadhi ya kucheza kama Mtanzania.

Akizungumzia suala hilo, Hersi ameeleza kuwa Yanga ilimsajili Damaro akiwa tayari ametambuliwa rasmi kama Mtanzania, huku taratibu zote za uraia wake zikisimamiwa na mamlaka husika za serikali, hususan Idara ya Uhamiaji.

“Yanga SC hatuhusiki na lolote kuhusu uraia wa Damaro. Tulimsajili akiwa tayari ameidhinishwa na Uhamiaji, na hata taarifa rasmi zilishatolewa zikimtambua kama Mtanzania. Alipata uraia mwaka 2025 akiwa na Singida BS kabla hajajiunga na Yanga,” amesema Hersi.

Ameongeza  kuwa wakati Yanga inamsajili mchezaji huyo kutoka Singida BS, leseni yake tayari ilikuwa ikimtambua kama Mtanzania, jambo ambalo pia linaonekana katika mfumo wa usajili wa kimataifa wa FIFA (TMS).

“Katika mfumo wa usajili, leseni inaonyesha wazi kama mchezaji ni wa kigeni au mzawa. Kwa Damaro, kila kitu kilikuwa kinaonyesha ni Mtanzania. Hivyo, kuhusisha Yanga na suala hili si sahihi, kwa sababu alitoka Singida BS akiwa tayari amesajiliwa kama mchezaji wa ndani,” amesisitiza.

Yanga imeeleza kuwa ilifuata taratibu zote za usajili kwa kuzingatia nyaraka rasmi zilizothibitishwa na mamlaka husika, na haikushiriki kwa namna yoyote katika mchakato wa kumpatia Damaro uraia wa Tanzania.

SIO SIMBA SIO YANGA VITA YA CHOBWEDO YAPAMBA MOTO SOWAH NJIANI KUTOKA, SIMBA KUWINDA MBADALA WAKE