Home Habari za michezo SIMBA WATINGA SOKONI, WAMLENGA NYOTA WA MADEAMA

SIMBA WATINGA SOKONI, WAMLENGA NYOTA WA MADEAMA

0

UONGOZI wa klabu ya Simba unaendelea kujiimarisha kuelekea msimamo ujao kwa kuanza kuweka rada zake kwa wachezaji wenye uwezo mkubwa barani Afrika.

Imeelezwa kywa kuwa wanafikiria kumsajili kiungo mahiri Salim Adam’s anayekipiga katika klabu ya Medeama SC ya Ghana.

Adams amekuwa katika kiwango bora msimu huu, akionesha uwezo mkubwa wa kufunga na kusaidia timu yake katikati ya uwanja, katika mechi 25 alizocheza, amefanikiwa kufunga mabao 9 huku akitoa asisti moja, takwimu zinazomfanya kuwa mmoja wa viungo hatari zaidi kwa sasa katika ligi ya Ghana.

Mbali na mchango wake wa mabao, kiungo huyo pia ameonyesha ubora wa hali ya juu kwa kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi mara saba, jambo linalodhihirisha namna anavyokuwa na ushawishi mkubwa ndani ya kikosi chake kila anapocheza.

Iwapo dili hilo litakamilika, basi Simba SC itakuwa imeongeza nguvu kubwa katika safu ya kiungo, hasa ikizingatiwa mahitaji ya timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Hata hivyo, Simba  haijawekwa wazi iwapo mazungumzo rasmi tayari yameanza kati ya pande husika licha ya kusema kuwa wameanza kufanya usajili mapema kulingana na nafasi  kocha wao, Steve Backer amewapendekeza kwa lengo la kuimarisha kikosi chao.

Adams anaendelea kung’ara nchini Ghana, huku macho ya mashabiki wa soka yakisubiri kuona hatma yake iwapo ataungana na wekundu hao wa Msimbazi au ataendelea kusalia Medeama SC kwa muda zaidi