Home Habari za michezo VITA YA UBINGWA EPL KUAMULIWA LEO MANCHESTER CITY, ARSENAL

VITA YA UBINGWA EPL KUAMULIWA LEO MANCHESTER CITY, ARSENAL

0

Leo tarehe 19 kuanzia saa 18:30 kwenye uwanja wa Etihad utashuhudia moja ya mechi zenye uzito mkubwa katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza, ambapo Manchester City watakuwa wenyeji wa Arsenal katika pambano linalotazamiwa kuamua timu itakayotwaa ubingwa msimu huu .

 

Arsenal wanaingia uwanjani wakiwa kileleni mwa msimamo kwa pointi 70 baada ya mechi 32, huku Manchester City wakiwa na pointi 64 baada ya mechi 31, wakiwa na mechi moja mkononi na tofauti ya pointi sita pekee .

Katika mechi za hivi karibuni kati ya timu hizi, Arsenal wameshinda mara 87, City mara 54, huku sare zikiwa 46 katika mechi 187 za Ligi Kuu na mashindano mengine . Mechi ya mwisho kati ya timu hizi ilikuwa Fainali ya Kombe la Carabao mnamo Machi 22, 2026, ambapo Manchester City waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwa nyundo za Nico O’Reilly, jambo linaloipa timu ya Pep Guardiola kijiamini zaidi.

Kwa mujibu wa takwimu za msimu huu, Manchester City wamekuwa na rekodi nzuri nyumbani wakiwa wameshinda mechi 11 kati ya 15, sare 3 na kupoteza mara 1 tu, wakiwa wamefunga mabao 36 na kufungwa 11. Arsenal wakiwa ugenini wameshinda mechi 9 kati ya 16, sare 5 na kupoteza 2, wakiwa wamefunga mabao 26 na kufungwa 13.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Katika msimamo wa sasa, Arsenal wanaongoza kwa pointi 70, huku Manchester City wakiwa na pointi 64 lakini wakiwa na mechi moja mkononi, hivyo ushindi wa City utawasawazisha kwa pointi huku Arsenal wakiwa na tofauti ya mabao mengi.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, akiwategemea wachezaji wake muhimu Erling Haaland, Antoine Semenyo Nico O’Reilly ambao wa mamekuwa na muendelezo wa viwango vyao.

Kwa upande wa Arsenal, kocha Mikel Arteta anawakosa wachezaji wawili muhimu Martin Odegaard na Bukayo Saka  jambo linalopunguza ubunifu wa safu ya kiungo, huku Viktor Gyökeres akiwa mfungaji bora wa timu kwa mabao 12 msimu huu.

Katika michezo ya hivi karibuni ya Ligi Kuu, City wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea ugenini (Aprili 12), huku Arsenal wakipata kipigo cha nyumbani cha 2-1 mikononi mwa Bournemouth (Aprili 11). Jisajili