Habari za michezo
ALIYEIPA SIMBA ALAMA MOJA KARIAKOO DERBY AVUNJA UKIMYA
Vardo
May 4, 2026
9:23 am
BEKI wa Yanga SC, Israel Mwenda, amekiri hadharani kufanya kosa kazini lililoigharimu timu yake katika mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Simba SC uliomalizika kwa sare ya 2-2.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Mwenda aliamua kusemaย ukweli mchungu kwa mashabiki wa Wananchi, akichukua lawama zote kwa matokeo ya mchezo huo.
Kwa masikitiko makubwa, Mwenda aliweka ujumbe uliogusa hisia za wengi, amesisitiza kuwa hatotafuta kisingizio chochote kwa yaliyotokea uwanjani.
โSiku na siku nzuri kazini nimekosea na kuigharimu timu, nimewaangusha wachezaji wenzangu na mashabiki na nipo tayari kupokea lawama zote kutoka kwa mashabiki, ishara ya ukomavu na uwajibikaji,” amesema Mwenda.
Beki huyo ameonyesha kuumizwa na namna juhudi za Wananchi zilivyokwenda bila malipo kwenye pambano hilo la watani wa jadi dimbani Mbweni.
โWananchi hamkustahili kuona juhudi zenu na sapoti zikiishia bila furaha,โ amesema Mwenda.
Licha ya maumivu ya kuikosesha timu yake ushindi, Mwenda hakukata tamaa, ameahidi kujifunza kutokana na kosa hilo na kurejea akiwa na makali zaidi.
โNimejifunza kwa makosa na ntapambana zaidi kurudi nikiwa bora kuliko leo,โ amesema beki huyo .