Safu ya kiungo ya United ilionekana kupoteza umbo, huku Casemiro na Mainoo wakisogea mbele kupita kiasi na kuacha ulinzi wazi. Baadaye, United walirejea kwenye mchezo na Mainoo akafunga bao la ushindi baada ya mpira uliorejeshwa na Amad.
Ushindi huo ulionyesha uimara wa kisaikolojia licha ya kuyumba kwa muda, jambo ambalo linaleta sura ya pili ya kikosi hicho, kwamba Carrick anakijenga kisaikolojia zaidi kuliko kimbinu kwani wachezaji haohao ndio ambao makocha Ruben Amorim na Erik Ten Hag waliwatumia, lakini waliambulia patupu uwanjani.
Ingawa kiwango chao cha kubadilika-badilika kinaweza kumtia wasiwasi Carrick, ushindi ni muhimu kwa sasa kwani umewahakikisha nafasi ya Ligi ya Mabingwa.
TAKWIMU MUHIMU
Kufuatia mchezo huo, kiungo wa Liverpool, Dominik Szoboszlai sasa amefikisha mabao 13 na asisti 10, akiwa mchezaji wa tatu kufikisha mabao 10+ na pasi zamabao 10+ msimu huu, baada ya Rayan Cherki wa Manchester City na Jarrod Bowen anayekipiga West Ham United, ambako amekuwa mtamu zaidi katika mechi hizi za mwisho mwisho.
Tangu kuondoka kwa Ruben Amorim, hakuna aliyefunga zaidi ya Benjamin Sesko aliyetupia bao lake la tisa kwenye Ligi Kuu England msimu huu na kumfanya kuwa mojawapo wa maingizo bora zaidi kwenye mashindano hayo, lakini yasiyoangaliwa kwa jicho la tatu la kuzisaidia timu wanazozichezea kwa ubora.
Kwa upande wa Liverpool watakuwa wameruhusu mabao 17 kutokana na mipira ya kutenga (set-pieces) msimu huu ikiwa ni rekodi yao mbaya zaidi katika misimu zaidi ya 10 iliyopita, jambo ambalo linawalazimu kurudi mezani kutafuta mafundi wa kukabiliana na mipigo hiyoya hatari kutoka katika timu zingine ili yaje yawaasaidie, kwani kadri misimu inavyokwenda kuanzia ujao huenda mambo yakawa magumu zaidi kwao.
Na ni kutokana na hilo, limechangia pia kwa Liverpool kupoteza mechi ya 18 msimu huu katika mashindano yote, jambo ambalo pia linatilia walakini katika namna timu hiyo inavyojilinda chini ya nahodha Virgil van Dijk. Kwa Man United hiyo ilikuwa ni mechi ya nane ya ushindi nyumbani kati ya tisa za Carrick akiwa na Manchester United msimu huu kwenye mashindano ya Ligi Kuu England.
MATOKEO EPL MECHI ZA WIKIENDI
Brentford 3-0 West Ham United
Newcastle United 3-1 Brighton
Wolves 1-1 Sunderland
Arsenal 3-0 Fulham
Bournemouth 3-0 Crystal Palace
Aston Villa 1-2 Tottenham