Kwa ujumla, timu hizo zimekutana mara 11 ndani ya ligi, Simba ikishinda kumi, wakati JKT Tanzania nayo imeshinda moja, hakuna sare baina yao.
MTIBWA VS DODOMA
Mechi ya Mtibwa Sugar ambayo ni mwenyeji wa Dodoma Jiji itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar kuanzia saa 2:30 usiku, Wakatamiuwa hao ndiyo wenye presha zaidi ya kupata matokeo ya ushindi ili kuondoka nafasi ya 11 waliyopo katika msimamo wa Ligi Kuu kabla ya mechi ya jana. Mtibwa imecheza mechi 20, imeshinda tano, sare nane, imepoteza saba, imefunga mabao 16, imeruhusu 24 na kukusanya pointi 23, huku Dodoma Jiji iliyocheza mechi 20, imeshinda sita, ina sare saba sawa na kupoteza, inamiliki mabao 18, imeruhusu 21, ina alama 25 katika nafasi ya nane kabla ya jana.
Nahodha wa Mtibwa, Oscar Masai, amesema: “Mechi itakuwa ngumu, tunahitaji ushindi ili kupanda nafasi za juu zaidi, hatutaki kurudi tulikotokea.”
Wakati kocha wa Dodoma Jiji, Aman Josiah akisema: “Ligi imefika pagumu, hakuna mechi nyepesi hasa kulingana nafasi tulizopo ambazo hakuna timu inaweza ikajihakikishia kusalia kwenye ligi, ni kama ushindani umebakia kwetu sisi wenyewe kwa wenyewe ukiondoa zile timu tatu za juu, pia haitakuwa mechi yenye mabao mengi hata ukicheza na timu iliyopo mkiani ngumu kupata mabao mengi, kikubwa ni kila kocha ana mbinu zake za kupata alama tatu na kuzuia usifungwe.”