WAKATI Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), ikitarajiwa kuanza Mei 16, mwaka huu, wachezaji 42 wa kimataifa wamesajiliwa katika timu tofauti, huku 23 wakiwa Wakongomani.
Kati ya wachezaji hao, 27 wamesajiliwa katika timu za wanaume, huku 15 wanawake. Majina hayo yaliyotolewa na uongozi wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), kwa timu zote 32 imeonyesha DRC Congo ndiyo iliyoongoza kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wakiwa ni 23.
Kocha wa kikapu kutoka Temeke, Pius John, alisema usajili huo wa nyota wa kimataifa umeonyesha ni jinsi Ligi ya Kikapu ya BDL inavyotambulika hadi nje ya nchi.
Orodha hiyo ipo hivi; Dar City kuna Shalom Ikidigwe (Nigeria), Elijah Mukelabai (Zambia), Chelk Bamba Diallo (Senegal) na Nkosinathi Sibanyoni (Afrika Kusini). Veins imemsajili Sam Agutu (Kenya), wakati DB Oratory wakiwa na James Omodi (Kenya) na Yang Ogweno (Kenya).
Kwa Stein Warriors kuna Daniel Kola (DR Congo), Moise Bukengu (DR Congo) na Spoican Ngoma (Zambia). Pazi imemsajili Rerry-Rostand (Gabon) na Samuel Luanda (DR Congo). Mlimani BC pia wapo David Buyamba (DR Congo), Jeancy Traore Bukas (DR Congo), Merva Cosma (DR Congo), Lukambala Kingumba (DR Congo) na Henock Manga (DR Congo).
Savio imewasajili Ntibonera Muteba (DR Congo) na Bofio Jephine (DR Congo), huku UDSM Outsiders ni Felix Muteba (DR Congo), Cell Ntambave (DR Congo), Bushiri Yumbi (DR Congo), Manu Mwamba (DR Congo) na Christiano Luanga (DR Congo). Vijana City Bulls kuna Soro Godfrey (Uganda), Philip Otieno (Kenya) na Nathan Kangudi (DR Congo).
Kwa upande wa wanawake, DB Lioness amesajiliwa Annetatiana Essama (Cameroon), Vijana Queens yupo Lisiane Ngomba (DR Congo), Aurelia Irebu (DR Congo) na Natalie Akinyi (Kenya). Pazi Queens ni Louange Cirhuza (DR Congo), Kavira Nzema (DR Congo), Kiyana Mbavumoja (DR Congo) na Sophia Omenda (Kenya).
DB Troncatti imewasajili Sakina Kakashi (DR Congo), Bamenge Marlibe (DR Congo) na Doreen Wanjaa (Kenya). Tausi Royals ni Divine Irakoze (Burundi). Reel Dreem wapo Dorcas Marondera (Zimbabwe), Evelne Nakinying (Uganda) na Ruth Atueheire (Uganda).