Habari za michezo

NANE KUCHUANA NUSU FAINSALI FA CUP, ZANZIBAR

Vardo May 11, 2026 6:32 pm

TIMU nne za Unguja na zingine nne za Pemba zimetinga nusu fainali ya Kombe la FA Zanzibar kuwania ubingwa huo unaoshikiliwa na KMKM.

Katika timu hizo nane, tatu pekee ndizo zinashiriki Ligi Kuu Zanzibar, huku zingine tano zikikitokea Ligi Daraja la Kwanza hali inayoonesha kumekuwa na ushindani wa kweli.

Zilizofuzu hatua hiyo upande wa Unguja ni JKU na KMKM zinazoshiriki Ligi Kuu huku za Ligi Daraja la Kwanza ni Raskazone na Black Sailors. Kwa Pemba, inayoshiriki Ligi Kuu ni Chipukizi pekee, wakati Mwenge, ChakeChake na Wawi Stars zikiwa Ligi Daraja la Kwanza.

JKU ndiyo timu ya kwanza kufuzu nusu fainali baada ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Kipanga.

Kule Pemba, mabingwa watetezi wa kombe hilo ukanda huo, Chipukizi United iliingia nusu fainali baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya New Stone Town.

KMKM ilijiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake baada ya kuifunga Mlandege mabao 2-1, huku Mwenge ikiitoa Fufuni kwa bao 1-0.

Raskazone iliiondosha KVZ kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1, wakati Black Sailors ikiitoa Mafunzo kwa penalti 3-2 baada ya sare ya bao 1-1.

Chakechake imefuzu hatua hiyo kwa kuitandika Machomane mabao 3-2 wakati Wawi Stars ikikamilisha hesabu kwa kuifunga Azimio.

SIMU MPYA INAKUSUBIRI *149*10# JUMATANO HII NA UWE MSHINDI LIVERPOOL YAITISHA CHELSEA KWA ALONSO