Habari za michezo

UBINGWA LIGI KUU ZANZIBAR, JKU NA UHAMIAJI KUPIGANA VIKUMBO

Vardo May 15, 2026 9:10 am

MECHI kati ya Uhamiaji na JKU itakayochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Mao B kisiwani Unguja, itakuwa yenye ushindani wa kusaka alama tatu zitakazoamua hatma yao ndani ya Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

Timu hizo zipo katika vita ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo ambapo mara ya mwisho kukutana katika mzunguko wa kwanza, JKU iiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mbali na vita ya uwanjani, kuna nyingine kati ya makocha wa timu hizo ambao walishawai kufanya kazi pamoja msimu wa 2024-2025.

Kocha Mkuu wa JKU, Ali Bakari Mgazija, alikuwa anaiongoza Uhamiaji wakati Abdul Saleh Mohammed akiwa msaidizi wake. Kwa sasa Mohammed ni kocha mkuu wa Uhamiaji.

Akizungumza na Soka la Bongo, Kocha wa Uhamiaji, Abdul Saleh, amesema wamejiandaa vya kutosha kuelekea katika mchezo huo na dhamira yao ni kuondoka na alama tatu.

Kocha huyo, amesema wanafahamu umuhimu wa kushinda mchezo wa leo na hasara za kupoteza, hivyo amewaambia wachezaji wacheze kwa tahadhari kubwa ndani ya dakika 90 ili kuibuka na ushindi.

“Tunaiheshimu JKU, lakini hatupo tayari kupoteza dhidi yao, kwa hiyo tutapambana kuvuna alama tatu,” amesema.

Naye, Kocha Mkuu wa JKU, Ali Bakari Mngazija, amesema mchezo utakuwa mgumu lakini wamejipanga kupambana kwa hali yoyote kuhakikisha wanashinda.

Mgazija amesema, malengo yao ni kuwa mabingwa msimu huu, hivyo ili kutimiza hilo, lazima ushinde ndiyo maana wanapambana kila mechi kupata matokeo mazuri.

Mbali ya kipute hicho, kutakuwa na mtanange mwingine katika uwanja wa Mao A, Unguja pale ambapo Zimamoto ikikabiliana na KMKM ikiwa ni vita ya kuwania kumaliza ndani ya nne bora na kuepuka kushuka daraja.

Mpaka sasa, JKU ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar ikiwa na alama 48, wakati Uhamiaji yenye alama 41, inashika nafasi ya nne, zote zikicheza mechi 24. Vinara ni KVZ wenye alama 52 baada ya mechi 25.

DABI YA KISASI NA MABINGWA WPL ANGEL NYIGU ALIVYOWAHESHIMISHA ZUCHU NA DIAMOND