Habari za michezo

PAUL PETER AFICHUA SIRI YA BAO LAKE

Vardo May 22, 2026 10:10 pm

UNAWEZA kushangaa bao kali alilofunga straika wa JKT Tanzania, Paul Peter dhidi ya Fountain Gate katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Mei 21, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, lakini nyuma ya tukio hilo, kuna simulizi ya kufurahisha.

Straika huyo ambaye alifunga bao hilo la kusawazisha katika sare ya 2-2, aliliambia Mwanaspoti kwa muda mrefu alikuwa na malengo ya kufunga bao kali kama hilo na alijaribu mara kadhaa msimu huu bila ya mafanikio kabla ya kupatia.

Peter ambaye ni mchezaji wa zamani wa Azam akiwahi pia kupita Mugabe FC ya Sinza jijini Dar, amesema alishindwa kidogo kufunga bao hilo kwenye mechi dhidi ya Yanga, Namungo, Simba na Mbeya City.

“Unajua siyo nilikuwa napanga kufunga bao kama hili lakini kuna wakati unapokea krosi ambayo inakupa akili uruke kama vile, msimu huu nilishakaribia kufunga kama vile lakini ikashindikana,” amesema Peter.

“Kuna mechi nazikumbuka nilikaribia kufunga kama vile dhidi ya Yanga, Namungo, Mbeya City na hata Simba, lakini ikashindikana, jana (Mei 21, 2026) Mungu akanisaidia nikafanikiwa kufunga.

“Kwanza nawapongeza wachezaji wenzangu, unajua wakati mwingine kabla ya mimi tunatakiwa kumshukuru aliyenipigia ile krosi ambayo ilinipa akili ya kuimalizia kwa mtindo ule,” amesema nyota huyo.

Straika huyo aliyefikisha mabao sita kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, amecheza mechi zote 24 ndani ya kikosi hicho huku bao lake dhidi ya Fountain Gate, alilifunga baada ya kupita takribani miezi sita.

Mara ya mwisho alifunga Novemba 29, 2025 ambapo pia alitikisa nyavu za Fountain Gate katika ushindi wa 2-0, akitupia yote. Pia ana asisti mbili. Mabao mengine ameyafunga dhidi ya Mashujaa, Azam na Mbeya City.

ODDS KUBWA NA USHINDI WA AJABU NA BET BOOST YA MERIDIANBET ELIUD AMBOKILE APATA MZUKA MPYA MBEYA CITY