Yanga SC
YANGA YAMUWINDA BITEGEKO KIMYA KIMYA
Vardo
May 24, 2026
9:36 am
KIGONGO kikubwa cha usajili kinaendelea kuwaka moto huku taarifa zikidai mabosi wa Yanga wameanza kufanya mawasiliano ya chini kwa chini kwa lengo la kuinasa sainiya kiungo mshambuliaji Adolf Bitegeko kutoka Azam FC, kuelekea dirisha kubwa la usajili wa msimu ujao.
Bitegeko ambaye kwa sasa anakitumikia kikosi cha Azam FC, anaripotiwa kubakiza miezi sita pekee kwenye mkataba wake, jambo linalompa nafasi ya kuanza kufanya mazungumzo na klabu nyingine kabla ya msimu mpya kuanza rasmi.
Inaelezwa kuwa Yanga wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mwenendo wa kiungo huyo kutokana na kiwango kizuri alichokuwa akikionyesha ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, hasa uwezo wake wa kutengeneza nafasi,
Taarifa zimeeleza kuwa nyota huyo anauwezo wa kusaidia mashambulizi na kucheza kwa ubunifu mkubwa katikati ya uwanja.
Bitegeko anaweza kuongeza ushindani mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga, hasa katika kipindi ambacho timu hiyo inaendelea kujipanga kupigania mataji ya ndani pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
Hadi sasa kuna taarifa iliyotolewa na Yanga SC wala Azam FC kuhusu mazungumzo hayo, huku macho ya mashabiki wengi yakielekezwa kuona hatma ya kiungo huyo katika kipindi hiki cha kuelekea dirisha jipya la usajili.