Michezo Bongo

PAUL PETER ANOGEWA KUTUPIA LIGI KUU

Vardo May 26, 2026 10:10 pm

MSHAMBULIAJI wa JKT Tanzania, Paul Peter amefanikiwa kufikia idadi ya mabao aliyofunga msimu uliopita ndani ya Ligi Kuu Bara na sasa ni kama amenogewa kufunga huku akisema anataka kuzitikisa nyavu zaidi kwenye mechi tano zilizosalia.

Mpaka sasa mshambuliaji huyo amefunga mabao manane kwenye Ligi Kuu Bara ambayo ni sawa na yale aliyoyafunga msimu uliopita, lakini pia akiwa na matano katika Kombe la Shirikisho (FA).

Akizungumza na Soka la Bongo, Peter amesema kwasasa baada ya kufikisha mabao hayo, anatamani kumaliza msimu akiwa na angalau mabao 10 au zaidi katika mechi ambazo zimesalia.

Peter amesema ubora wa kikosi kwa sasa anaamini hatua hiyo itatimia kutokana na mfumo wa uchezaji wao kuruhusu kufunga.

“Nikweli nimefikia idadi ya mabao ya msimu uliopita lakini jambo zuri ni kwamba msimu huu bado kuna mechi tano zimesalia ambazo kama Mungu akinipa afya naweza kufunga zaidi,” amesema Peter ambaye ni mchezaji wa zamani wa Azam FC.

“Nataka kumaliza msimu huu kwa kufunga angalau mabao 10 au ikiwezekana zaidi, uzuri ni kwamba timu yenyewe mfumo unaruhusu kufunga lakini pia namna tunavyocheza kwa ushirikiano na wachezaji wenzangu.” Aliongeza kuwa baada ya kulazimishwa sare  2-2 na Mtibwa Sugar, wanapambana kuhakikisha wanamaliza ndani ya tano bora katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

 

RISASI YAANZA VIZURI LIGI YA KIKAPU SHINYANGA LEO NI WEWE AU NANI..?JANGWANI PESA ZIMEJAA