Tetesi za usajili

MAN UNITED KUPINDUA MEZA KWA EDERSON

Vardo May 28, 2026 4:47 pm

Manchester United wako katika mazungumzo ya hatua za mwisho kumsajili kiungo wa Brazil wa Atalanta BC, Ederson, kuwa usajili wao wa kwanza wa majira ya joto.

Vyanzo mbalimbali vimeidai kuwa dili hilo liko karibu kukamilika, huku ada ya awali ya pauni 35milioni pamoja na nyongeza ya pauni 3 milioni ikitarajiwa kwa mchezaji huyo mwenye miaka 26.

Maofisa wakuu wa United wamepunguza uvumi huo na kusema bado hakuna makubaliano rasmi kwa Ederson, ambaye amebakiza miezi 12 kwenye mkataba wake.

Hata hivyo, siku ambayo walitangaza faida ya robo ya tatu ya pauni 37.7 milioni kwa miezi tisa hadi Machi 31, Mtendaji Mkuu Omar Berrada kusema alikuwa “na matumaini makubwa kuhusu maendeleo ya klabu” ni wazi kuwa United wanataka kumaliza zaidi ya nafasi ya tatu chini ya kocha mpya Michael Carrick.

United bado wanadaiwa kiasi kikubwa cha ada za usajili ambazo hazijalipwa, jambo linalounda sehemu kubwa ya pauni482 milioni zinazodaiwa katika “malipo ya biashara na mengineyo”, na linaonyesha kazi kubwa inayohitajika kurekebisha hali yao ya kifedha.

Lakini wameamua kubaki washindani kwenye soko la usajili huku wakiahidi kutorudia kosa la kutoa mikataba mirefu na yenye gharama kubwa kama walivyofanya zamani.

Man United wanaipa kipaumbele safu ya kiungo wa kati majira haya ya joto baada ya kuondoka kwa Casemiro na kutokuwa na uhakika kuhusu mustakabali wa Manuel Ugarte.

Andy Robertson

Tottenham Hotspur FC wako karibu kufikia makubaliano na beki wa kushoto wa Scotland, Andy Robertson baada ya kuondoka kwake Liverpool FC.

Mchezaji huyo mwenye miaka 32 alicheza mechi yake ya mwisho kwa Liverpool dhidi ya Brentford FC, baada ya kutangaza kuwa ataondoka klabuni hapo mkataba wake utakapoisha majira haya ya joto.

Tottenham, ambao wakati huo walikuwa wakiongozwa na Thomas Frank, walimlenga Robertson tangu dirisha la usajili la Januari.

Anthony Gordon

Barcelona wameelekeza macho yao kwa Anthony Gordon, klabu hiyo ya Catalonia tayari imefikia makubaliano na mchezaji huyo wa England, na sasa klabu hizo mbili zinajadili ada ya usajili ambayo inaweza kuwa kati ya milioni 70 hadi 80.

Uwepo wa Deco nchini England ulikuwa mahsusi kuzungumzia mustakabali wa Gordon, kwani Joan Laporta, Hansi Flick pamoja na Deco wanaamini kuwa Mwiingereza huyo anaweza kuwa usajili wenye uwezo mkubwa kwa klabu hiyo.

Elliot Anderson

Manchester City FC wanaipa kipaumbele dili la kumsajili kiungo wa Nottingham Forest FC na England, Elliot Anderson mwenye miaka 23 huku wakitafuta kuanza enzi mpya baada ya Pep Guardiola.

Yan Diomande

RB Leipzig wameweka wazi kuwa winga wa Ivory Coast, Yan Diomande mwenye miaka 19, ambaye analengwa na Liverpool FC, hataondoka majira haya ya joto baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Morgan Rogers

Mabingwa wa Ligi Kuu England, Arsenal wako tayari kuongeza juhudi zao za kumtaka nyota wa Aston Villa, Morgan Rogers.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anaongoza mwenyewe mpango wa kujaribu kumshawishi Rogers kuondoka Villa, mabingwa wa  Europa Ligi. Inaaminika kuwa mazungumzo ya awali tayari yamefanyika kati ya Arsenal na washauri wa mchezaji huyo.

Arsenal wanaweza kukutana na ushindani kutoka Chelsea FC huku mkurugenzi wa ufundi wa soka wa Manchester United FC Jason Wilcox pia akitajwa kuwa shabiki mkubwa wa Rogers.

Aaron Wan-Bissaka

Everton FC wanajiandaa kutoa ofa ya pauni10 milioni kwa ajili ya beki wa kulia, Aaron Wan-Bissaka kutoka West Ham United FC iliyoshuka daraja.

West Ham walimaliza safari yao ya miaka 14 katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kumaliza pointi mbili nyuma ya mstari wa usalama.

Inatarajiwa kuwa West Ham watapoteza baadhi ya wachezaji wao muhimu kufuatia kushuka daraja. Everton wameanza kuelekeza macho yaoLondon huku wakitathmini uwezekano wa kutoa pauni 10milioni kwa Wan-Bissaka.

WADAU WA KIKAOPU WAIPONGEZA DAR CITY SIMU MPYA INAKUSUBIRI PIGA *149*10# JUMATANO HII NA UWE MSHINDI