Azam FC

TEGISI ATAMANI KUCHEZA NA FEI TOTO AZAM FC

Vardo May 30, 2026 9:53 am

STRAIKA wa Pamba Jiji, Mathaw Tegisi amesema moja ya ndoto zake katika soka la kulipwa nchini ni kuitumikia Azam, huku akibainisha anatamani kucheza sambamba na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ ndani ya kikosi hicho.

Mbali na hilo, Tegisi amemtaja kiungo wa Simba, Clatous Chama kuwa moja ya nyota anaojifunza mengi kutoka kwake.

Tegisi raia wa Kenya, msimu huu amekuwa na kiwango bora akiwa kinara wa ufungaji ndani ya Pamba Jiji akipachika mabao saba katika michezo 15 ya Ligi Kuu Bara aliyocheza.

Nyota huyo wa zamani wa Shabana FC na mfungaji bora wa timu hiyo ya Ligi Kuu nchini Kenya, ameendelea kuonesha ubora wake akihusika katika mabao 10 ndani ya Pamba Jiji na kuiweka nafasi ya saba kwa pointi 33. Akizungumza na Mwanaspoti, Tegisi amesema anavutiwa na ubora wa ligi ya Tanzania yenye vipaji kwa wachezaji, akimtaja Feisal Salum ‘Fei Toto’ kumvutia zaidi akieleza kutamani kuch eza naye.

Amesema tangu akiwa kwao nchini Kenya, amekuwa akivutiwa na soka la Azam FC akieleza kuwa hadi sasa anajifunza mengi kwa wachezaji akiwamo Chama wa Simba kutokana na pasi zake na unyumbulifu.

“Kwa pasi za macho zenye ubora ni Chama, lakini navutiwa na Fei Toto kwa kipaji alichonacho, nikifanya naye kazi tutakimbiza sana, isitoshe ninavutiwa na Azam kuanzia uwanjani hadi nje ya uwanja,”  amesema straika huyo.

Kuhusu vita ya ufungaji mabao, Mkenya huyo amesema kama isingekuwa ni majeraha aliyopata hadi kumkosesha michezo kumi, huenda angekuwa katika mnyukano na kinara wa mabao kwa sasa, Fei Toto mwenye 14.

Amesema anatumia vyema nafasi aliyonayo Pamba Jiji kama daraja la kumfikisha katika ndoto zake akieleza kuwa kwa sasa anaipambania timu kusaka nafasi nne za juu.

“Mechi 10 nilizokosa kutokana na majeraha huenda ningekuwa katika vita ya ufungaji bora, nakumbuka hata Kenya nilicheza nusu msimu nikafunga mabao 12 nikiachwa na kinara aliyefunga 16,”  amesema nyota huyo.

VIWANJA UGENINI KAA LA MOTO LIGI KUU BARA