Yanga SC

JAMBO JIPYA YANGA SC, MGONGANO WA VIWANJA WATIKISA MECHI DHIDI YA AZAM FC

Vardo June 3, 2026 1:20 pm

UONGOZI wa Yanga SC umeweka wazi kuwa unakabiliwa na changamoto ya ratiba iliyobana, hali inayowalazimu kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC.

Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Juni 2, 2026, ambapo Yanga SC watakuwa wenyeji, sasa umeingia kwenye mjadala baada ya mipango ya ratiba kuleta mgongano wa matumizi ya viwanja.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, klabu hiyo imejikuta ikilazimika kuachana na matumizi ya uwanja wa KMC Complex kutokana na ratiba kugongana na ratiba ya KMC FC.

Kamwe amesema hatua hiyo imewalazimu kuanza mchakato wa haraka wa kutafuta uwanja mbadala ili kuhakikisha mchezo huo unachezwa bila usumbufu wowote wa kiutendaji.

Ameeleza kuwa Yanga SC haikuwa na mpango wa kubadilisha uwanja, lakini mazingira ya ratiba yamewalazimisha kufanya marekebisho hayo muhimu kwa ajili ya uendeshaji wa ligi.

“Tunaenda kutangaza uwanja wa mechi yetu dhidi ya Azam FC. Siku hiyo ambayo tunacheza na Azam FC, KMC FC nao watakuwa na mechi yao, hivyo watatumia uwanja wao,” amesema Kamwe.

Hata hivyo, Yanga SC wamebainisha kuwa wanaendelea kushirikiana na mamlaka husika za ligi kuhakikisha ratiba inabaki kuwa rafiki, huku wakisisitiza kuwa lengo ni kumaliza msimu kwa wakati bila kuathiri ubora wa mashindano.

SIMBA WATAMBA, SAA NANE MCHANA SIO TATIZO ONGEZA ODDS ZAKO PAPO PAPO NA LIVE IN PAY-PLAY BOOSTER YA MERIDIANBET