news

WABUNGE WALIOSAFIRI MOROCCO BILA KIBALI, ZUNGU AWAPA SIKU NNE WAJIELEZE

Vardo June 4, 2026 2:02 pm

Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu ametoa siku nne kwa wabunge waliokwenda Morocco bila kibali cha Spika wajieleze huku akitoa onyo kwa wabunge watoro bungeni.

Wabunge hao ni sehemu ya mashabiki waliokwenda Morocco kushuhudia fainali ya Mataifa Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kati ya Serengeti Boys ya Tanzania na Senegal.

Mechi hiyo ilichezwa katika Uwanja Uwanja wa Prince Moulay Hassan, Rabat na vijana wa Senegal kuibuka na ushindi wa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Spika Zungu ametoa agizo hilo leo Alhamisi, Juni 4, 2026, bungeni jijini Dodoma akimtaka Katibu wa Bunge kuwaandikia barua mara moja na wajibu vinginevyo hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Mbali na waliokwenda Morocco, Spika Zungu amesema kumekuwa na utoro ndani ya Bunge ambao hauwezi kuvumiliwa wakiwemo wengine kusalimiana.

“Lakini mawaziri nao wanaondoka wote, najua wana vibali vyao lakini Waziri Mkuu, hawa wasipewe vibali vya ziara wote, akitoka waziri basi naibu awepo Bungeni siyo wanakosekana wote,” amesema Zangu.

Kingine amebainisha kuna baadhi ya wabunge wanaomba vibali wakisema wanakwenda majimboni lakini wanakwenda nje ya nchi.

NYUMA YA YANGA KWA ALAMA MBILI, BARKER BADO ANAAMINI SIMBA KUTWAA UBINGWA TAIFA STARS YAPATA PIGO MOROCCO