Habari za michezo

HAKIMI AONYESHA UJASIRI KUIKABILI KESI YA UBAKAJI, ATULIZA PRESHA MOROCCO

Vardo June 19, 2026 6:37 pm

Nahodha wa Morocco, Achraf Hakimi ameishusha presha timu yake ya taifa, saa chache kabla ya kuivaa Scotland baada ya kusema kuwa uamuzi wa mahakama ya Ufaransa kuhusu tuhuma zake za kubaka haumpi wasiwasi na haumtoi mchezoni.

Kauli hiyo ya Hakimi imekuja muda mfupi baada ya rufaa yake ya kuomba shauri hilo juu ya tuhuma zake za kubaka zitupiliwe mbali.

Taarifa hizo zilihofiwa kwamba zingeweza kuharibu utulivu wa kambi ya Morocco inayojiandaa na mechi hiyo ya pili dhidi ya Scotland lakini Hakimi amewataka wenzake wawe na utulivu.

“Leo  stori ambayo sio yangu inazungumzwa kwa gharama ya familia yangu, maisha yangu na zaidi ya hapo. Kuna wakati najihisi nimekuwa mlenga rahisi.

“Nimekuwa nikisubiria kusimama kizimbani tangu siku ya kwanza. Na sasa nipo tayari kwa hilo. Nitakuwa na uwezo wa kuzungumza hadharani,” amesema Hakimi.

Hakimi amesema kuwa kwa muda mrefu ameamua kukaa kimya ili kutoa fursa kwa mamlaka za kisheria kuendelea na uchunguzi juu ya suala hilo.

Tuhuma hizo kwa Hakimi zilianza Machi 2023 ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 24 alipomtuhumu beki huyo kuwa alimbaka nyumbani kwake, jijini Paris.

Hata hivyo Hakimi ameonekana kukanusha hilo na amesema kuwa yuko tayari kujitetea kwa vile hakuwahi kufanya jambo hilo.

MVUTANO URENO? DADA WA RONALDO AIBUA TAHARUKI MPYA USA USO KWA USO DHIDI YA AUSTRALIA VITA YA KUNDI D