Simba SC

Simba Wajipa Kazi Moja Tu, Azam Fc Kazi Wanayo

Vardo July 3, 2026 8:41 am

BAADA ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba sasa imehamishia nguvu zake zote katika Kombe la Shirikisho la CRDB, ikilenga kumaliza msimu kwa kutwaa taji hilo.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema kikosi hicho kimejipanga kuhakikisha hakifanyi makosa katika mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC.

Simba inatarajiwa kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, Julai 4, 2026, huku ikihitaji ushindi ili kuhitimisha msimu kwa mafanikio.

Ahmed amesema mara baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya KMC FC, uongozi ulikutana na wachezaji na kufanya tathmini ya msimu uliomalizika.

Amesema katika kikao hicho waliwaeleza wachezaji kuwa licha ya kukosa ubingwa wa ligi, bado wana nafasi ya kuipa Simba furaha kwa kutwaa Kombe la Shirikisho la CRDB.

“Wachezaji tumeshawaambia ubingwa wa ligi tumekosa, lakini kwenye Kombe la Shirikisho la CRDB hatutaki kufanya makosa. Twendeni tukapambane na kuipigania furaha ya Simba pamoja na heshima ya nembo ya klabu yetu,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa wachezaji wamepokea ujumbe huo kwa uzito na wameonyesha utayari wa kupambana katika fainali ya Gombani, wakiamini wana uwezo wa kuhitimisha msimu kwa kutwaa taji hilo.

Hersi Aionya Simba, Tano Sio Mwisho, Zingine Zinakuja Yanga Wamtaka Akaminko Kuimarisha Safu Ya Kiungo