Simba SC

Mo Dewji Afungua Mfuko, Aahidi Simba Kali Kuliko Msimu Ujao

Vardo July 6, 2026 9:51 am

MWEKEZAJI wa Simba SC, Mohammed Dewji (Mo Dewji), ameahidi kuendelea kuimarisha kikosi cha timu hiyo kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi, akisisitiza lengo lao ni kuijenga Simba kuwa tishio zaidi katika msimu ujao wa mashindano.

Mo Dewji amesema dhamira kubwa ya uongozi ni kuhakikisha Simba inafanya vizuri katika mashindano ya ndani na hatimaye kutimiza ndoto ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF).

Amewapongeza mashabiki wa Simba kwa uaminifu na kujitoa kwao katika kipindi chote ambacho timu haikuwa ikitwaa mataji, akiwahakikishia kuwa msimu ujao utakuwa wa mafanikio na furaha kwao.

“Dhamira yetu ni kuona Simba inaendelea kufanya vizuri katika mashindano ya ndani na siku moja inatwaa ubingwa wa Afrika. Ili kufikia lengo hilo ni lazima tuwe na kikosi bora chenye wachezaji wenye uwezo wa kutimiza ndoto hiyo,” amesema Mo Dewji.

Kauli hiyo aliitoa kwa njia ya simu alipokuwa akizungumza na maelfu ya mashabiki wa Simba waliokusanyika katika Fukwe za Coco, jijini Dar es Salaam, kusherehekea ubingwa wa Kombe la Shirikisho, baada ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.

Sherehe hizo zilitanguliwa na gwaride la ubingwa lililopita katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kabla ya kuhitimishwa kwa mkusanyiko mkubwa wa mashabiki katika Fukwe za Coco.

Wewe Ndiwe Legend Ajaye? Evoplay Summer Season of Legends Inakupa Majibu Vita Za Usajili Zaanza Kuchacha, Simba, Yanga Mtu Kati Nyota Sauz