Simba SC

Nkeng Awekwa Katika Mpango Wa Simba Kagame, Barker Atamani Huduma Yake

Vardo July 7, 2026 6:35 pm

WAKATI mazungumzo kati ya Simba SC na mshambuliaji wa Stade Malien ya Mali, Taddeus Nkeng, yakiendelea kushika kasi, nyota huyo anatajwa kuwa sehemu ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kitakachoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2026/27.

Simba inatarajiwa kuanza kambi mwishoni mwa mwezi Julai kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya CECAFA Kagame 2026 pamoja na mashindano mengine ya msimu mpya, huku uongozi ukiendelea kukamilisha usajili wa wachezaji wanaoonekana kuwa na uwezo wa kuongeza nguvu ndani ya kikosi.

Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo kati ya Simba na Nkeng yamefikia hatua nzuri, huku mshambuliaji huyo akiwa miongoni mwa chaguo la benchi la ufundi la timu hiyo katika harakati za kuimarisha safu ya ushambuliaji.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mazungumzo hayo, ingawa makubaliano ya mwisho bado hayajakamilika, pande zote zinaonyesha nia ya kufikia muafaka ndani ya muda mfupi.

“Nkeng ni mmoja wa washambuliaji waliovutia benchi la ufundi la Simba linaloongozwa na Steve Barker kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao na kucheza katika nafasi tofauti za ushambuliaji. Ana sifa ambazo timu inazihitaji kuelekea msimu mpya,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa Simba inalenga kukamilisha usajili huo kabla ya kuanza rasmi kwa maandalizi ya msimu, huku michuano ya CECAFA Kagame ikitarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kukijenga kikosi na kukiandaa kwa mashindano ya ndani na kimataifa.

Iwapo dili hilo litakamilika, Nkeng ataingia kwenye orodha ya wachezaji wapya watakaoongeza ushindani ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, sambamba na nyota watakaobaki kutoka msimu uliopita.

Uongozi wa Simba unaendelea na mipango ya kukiboresha kikosi katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuunda timu yenye ushindani mkubwa itakayowania mataji ya ndani na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa msimu wa 2026/27.

Hazisubiri, Diamond Jackpot Inabadilisha Kila Dakika Kuwa Fursa Switzerland dhidi ya Colombia Nani kwenda Robo Fainali