Yanga SC

Baada Ya Mvutano, Fountain Gate Yakubali Kumuachia Abushiri Yanga

Vardo July 9, 2026 7:04 pm

KLABU ya Yanga inatajwa kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo mshambuliaji Juma Abushiri kutoka Fountain Gate kwa mkataba wa miaka mitatu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2026/27.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Abushiri anatarajiwa kusaini mkataba wenye thamani ya Sh30 milioni kwa kipindi cha miaka hiyo mitatu, huku akidaiwa kulipwa mshahara wa Sh5 milioni kwa mwezi.

Mazungumzo kati ya Yanga na Fountain Gate yalielezwa kuchukua muda kutokana na mchezaji huyo kuwa na mkataba wa muda mrefu wa miaka mitano na klabu yake. Hata hivyo, pande hizo zinadaiwa kufikia mwafaka, jambo lililofungua njia ya nyota huyo kuhamia Jangwani.

Awali, Fountain Gate ilikuwa ikielezwa kutokuwa tayari kumuuza Abushiri kwa klabu za ndani, ikisisitiza kuwa ilikuwa na mpango wa kumpeleka kucheza soka la Ulaya. Hata hivyo, taarifa za sasa zinaonyesha Yanga imefanikiwa kumshawishi mchezaji huyo na kufikia makubaliano ya uhamisho wake.

Abushiri atakuwa miongoni mwa nyongeza muhimu katika kikosi cha Yanga kinachojiandaa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kushiriki mashindano ya kimataifa katika msimu wa 2026/27.

Ulimwengu wa Pipi na Mamilioni ya Fursa Upo Kwenye Candy Treasures 3 Reels Sportpesa Yamkabidhi Mjasiriamali Milioni 286.6 Za Mid-Week Jackpot