Simba SC

Simba, Yanga Kufungua Rasmi Msimu Kwa Ngao Ya Jamii Agosti 12

Vardo July 9, 2026 6:52 pm

MSIMU mpya wa mashindano wa 2026/27 utafunguliwa rasmi Agosti 12 kwa mchezo wa Ngao ya Jamii utakaowakutanisha watani wa jadi, Simba SC na Yanga SC, katika pambano linalotarajiwa kuwasha moto wa ushindani mapema.

Mchezo huo utawakutanisha mabingwa wawili wa soka la Tanzania waliotawala mashindano ya ndani msimu uliopita, huku ukitarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi kutokana na historia na ushindani mkubwa uliopo kati ya vigogo hao wa Kariakoo.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema baada ya mchezo huo, pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2026/27 litafunguliwa rasmi Agosti 14.

Karia ameeleza kuwa ratiba kamili ya ligi itatangazwa mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa upangaji wa mechi, huku maandalizi ya msimu mpya yakiendelea katika hatua za mwisho.

Kutangazwa kwa tarehe hizo kumewaongezea hamasa mashabiki wa soka nchini, ambao sasa wanaanza kuhesabu siku kuelekea mwanzo wa msimu mpya, huku pambano la Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga likitarajiwa kuwa mwanzo wa mbio za kuwania mataji ya ndani katika msimu wa 2026/27.

Moalin Awaacha Viongozi Wa Yanga Kwenye Uamuzi Mgumu Ulimwengu wa Pipi na Mamilioni ya Fursa Upo Kwenye Candy Treasures 3 Reels