Michezo Bongo

Sportpesa Yamkabidhi Mjasiriamali Milioni 286.6 Za Mid-Week Jackpot

Vardo July 9, 2026 7:12 pm

Mjasiriamali wa Vikindu jijini Dar es Salaam, Latifah Hamisi Mdoka (28), amekuwa mshindi mpya wa Mid-Week Jackpot ya SportPesa Tanzania baada ya kujishindia Sh268,671,530, ushindi unaotarajiwa kubadili maisha yake na ya familia yake.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo jana jijini Dar es Salaam, Latifah alisema hakutarajia kushinda kiasi hicho kikubwa na kwamba alidhani simu ya kumtaarifu ushindi huo ilikuwa ya utani.

“Nilipopigiwa simu na kuambiwa nimeshinda, sikutegemea kabisa. Nimekuwa nikicheza jackpot kwa matumaini kwamba siku moja ningekuwa mshindi, na leo ndoto yangu imetimia. Namshukuru Mungu na SportPesa kwa ushindi huu ambao naamini utabadilisha maisha yangu na ya familia yangu,” alisema.

Latifah, ambaye ni mzaliwa wa Mchinga mkoani Lindi, alijiunga na SportPesa mwaka 2019 na amekuwa akishiriki mara kwa mara kwenye Mid-Week Jackpot na Supa Jackpot. Kabla ya ushindi huo aliwahi kujishindia bonasi ndogo, lakini huu ndio ushindi mkubwa zaidi katika historia yake.

Kwa mujibu wa SportPesa Tanzania, Latifah ni mshindi wa tano mkubwa wa jackpot mwaka 2026 na mwanamke wa tatu kujishindia jackpot ya mamilioni kupitia kampuni hiyo mwaka huu.

Mkuu wa Idara ya Masoko wa SportPesa Tanzania, Tracy Humplick, alisema ushindi wa Latifah unaonyesha kuwa uvumilivu na ushiriki wa mara kwa mara unaweza kuzaa matunda.

“Latifah amekuwa nasi kwa zaidi ya miaka saba na ameendelea kushiriki kwa uvumilivu. Leo ameona matokeo yake. Huu ni uthibitisho kuwa kila anayeshiriki ana nafasi ya kushinda, na tunafurahi kuona ushindi huu ukibadilisha maisha yake,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas, alisema tangu kampuni hiyo ilipoanza shughuli zake nchini, imewazawadia washindi wakubwa 29 wa jackpot wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 8.8.

Alisema ushindi wa Latifah unaongeza idadi ya wanawake wanaonufaika na jackpot za SportPesa na kudhihirisha kuwa washindi wanatoka katika maeneo na kada mbalimbali nchini.

“Tutaendelea kuwapa Watanzania fursa ya kujishindia zawadi kubwa kupitia bidhaa zetu mbalimbali na kubadilisha maisha yao,” alisema Tarimba.

Baada Ya Mvutano, Fountain Gate Yakubali Kumuachia Abushiri Yanga